Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 49

1Nisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili, 2 ninyi mataifa mlio mbali: 1 Kabla sijazaliwa, Bwana aliniita, 2 tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu. 1

2Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, 2 katika uvuli wa mkono wake akanificha; 1 akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa, 2 na kunificha katika podo lake. 1

3Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu, 2 Israeli, ambaye katika yeye 2 nitaonyesha utukufu wangu.” 1

4Lakini nilisema, “Nimetumika bure, 2 nimetumia nguvu zangu bure bila faida. 1 Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa Bwana, 2 nao ujira wangu uko kwa Mungu wangu.” 1

5Sasa Bwana asema: 2 yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake, 1 kumrudisha tena Yakobo kwake 2 na kumkusanyia Israeli, 1 kwa maana nimepata heshima machoni pa Bwana, 2 naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu; 1

6yeye asema: 1 “Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu 2 ili kurejeza makabila ya Yakobo, 2 na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi? 1 Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa, 2 ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.” 1

7Hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye Mkombozi na Aliye Mtakatifu wa Israeli, 1 kwake yeye aliyedharauliwa na kuchukiwa na taifa, 2 kwa mtumishi wa watawala: 1 “Wafalme watakuona na kusimama, 2 wakuu wataona na kuanguka kifudifudi, 1 kwa sababu ya Bwana, aliye mwaminifu, 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, aliyekuchagua wewe.” 1 Kurejezwa Kwa Israeli

8Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Wakati wangu uliokubalika nitakujibu, 2 nami katika siku ya wokovu nitakusaidia; 1 nitakuhifadhi, nami nitakufanya 2 kuwa agano kwa ajili ya watu, 1 ili kurudisha nchi 2 na kugawanyia urithi tena wale waliokuwa ukiwa, 1

9kuwaambia mateka, ‘Tokeni nje,’ 2 nao wale walio gizani, ‘Kuweni huru!’ 1 “Watajilisha kando ya barabara 2 na kupata malisho yao juu ya kila kilima kilicho kitupu. 1

10Hawataona njaa wala kuona kiu, 2 wala hari ya jangwani au jua halitawapiga. 1 Yeye mwenye huruma juu yao atawaonyesha njia, 2 na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji. 1

11Nitaifanya milima yangu yote kuwa barabara, 2 na njia kuu zangu zitainuliwa. 1

12Tazama, watakuja kutoka mbali: 2 wengine kutoka kaskazini, wengine kutoka magharibi, 2 wengine kutoka nchi ya Sinimu.” + 49:12 Sinimu hapa ina maana ya Aswani. 1

13Pigeni kelele kwa furaha, enyi mbingu; 2 furahi, ee dunia; 2 pazeni sauti kwa kuimba, enyi milima! 1 Kwa maana Bwana anawafariji watu wake, 2 naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa. 1

14Lakini Sayuni alisema, “ Bwana ameniacha, 2 Bwana amenisahau.” 1

15“Je, mama aweza kumsahau mtoto 2 aliyeko matitini mwake akinyonya, 1 wala asiwe na huruma 2 juu ya mtoto aliyemzaa? 1 Ingawa anaweza kusahau, 2 mimi sitakusahau wewe! 1

16Tazama, nimekuchora kama muhuri 2 katika vitanga vya mikono yangu, 2 kuta zako zi mbele yangu daima. 1

17Wana wako wanaharakisha kurudi, 2 nao wale waliokuteka wanaondoka kwako. 1

18Inua macho yako ukatazame pande zote: 2 wana wako wote wanakusanyika na kukujia. 1 Kwa hakika kama vile niishivyo, 2 utawavaa wote kama mapambo, 1 na kujifunga nao kama bibi arusi,” 2 asema Bwana. 1

19“Ingawa uliangamizwa na kufanywa ukiwa, 2 na nchi yako ikaharibiwa, 1 sasa nafasi itakuwa finyu kwa ajili ya watu wako, 2 nao wale waliokuangamiza watakuwa mbali sana. 1

20Watoto waliozaliwa wakati wa msiba wako 2 bado watakuambia, 1 ‘Mahali hapa ni finyu sana kwetu, 2 tupe eneo kubwa zaidi la kuishi.’ 1

21Ndipo utasema moyoni mwako, 2 ‘Ni nani aliyenizalia hawa? 1 Nilikuwa nimefiwa, tena tasa; 2 nilikuwa nimehamishwa na kukataliwa. 2 Ni nani aliyewalea hawa? 1 Niliachwa peke yangu, 2 lakini hawa wametoka wapi?’ ”

22Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: 1 “Tazama, nitawaashiria watu wa Mataifa, 2 nitainua bendera yangu kwa mataifa; 1 watawaleta wana wako mikononi yao, 2 na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao. 1

23Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea, 2 na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea. 1 Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa ardhi; 2 wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako. 1 Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana; 2 wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.” 1

24Je, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita, 2 au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?

25Lakini hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Naam, mateka watachukuliwa kutoka kwa mashujaa, 2 na nyara zitapokonywa kutoka kwa watu wakali. 1 Nitashindana na wale wanaoshindana nawe, 2 nami nitawaokoa watoto wako. 1

26Nitawafanya wale wanaokuonea kula nyama yao wenyewe, 2 watalewa kwa damu yao wenyewe, 2 kama vile kwa mvinyo. 1 Ndipo wanadamu wote watajua 2 ya kuwa Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako, 2 Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

← Isaiah 48Read In The App, Free →Isaiah 50 →

Study Isaiah 49

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566