Isaiah 60
1“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja 2 na utukufu wa Bwana umezuka juu yako. 1
2Tazama, giza litaifunika dunia 2 na giza kuu litayafunika mataifa, 1 lakini Bwana atazuka juu yako 2 na utukufu wake utaonekana juu yako. 1
3Mataifa watakuja kwenye nuru yako 2 na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako. 1
4“Inua macho yako na utazame pande zote: 2 Wote wanakusanyika na kukujia, 1 wana wako wanakuja toka mbali, 2 nao binti zako wanabebwa mikononi. 1
5Ndipo utatazama na kutiwa nuru, 2 moyo wako utasisimka na kujaa furaha, 1 mali zilizo baharini zitaletwa kwako, 2 utajiri wa mataifa utakujilia. 1
6Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako, 2 ngamia vijana wa Midiani na Efa. 1 Nao wote watokao Sheba watakuja, 2 wakichukua dhahabu na uvumba 2 na kutangaza sifa za Bwana. 1
7Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, 2 kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia, 1 watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu, 2 nami nitalipamba Hekalu langu tukufu. 1
8“Ni nani hawa warukao kama mawingu, 2 kama hua kuelekea kwenye viota vyao? 1
9Hakika visiwa vinanitazama, 2 merikebu za Tarshishi + 60:9 Au: za biashara (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 2:16 ). ndizo zinazotangulia, 1 zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, 2 wakiwa na fedha na dhahabu zao, 1 kwa heshima ya Bwana, Mungu wenu, 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, 2 kwa maana amekujalia utukufu. 1
10“Wageni watazijenga upya kuta zako, 2 na wafalme wao watakutumikia. 1 Ingawa katika hasira nilikupiga, 2 lakini katika upendeleo wangu 2 nitakuonyesha huruma. 1
11Malango yako yatakuwa wazi siku zote, 2 kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku, 1 ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa: 2 wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi. 1
12Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia; 2 utaharibiwa kabisa. 1
13“Utukufu wa Lebanoni utakujilia, 2 msunobari, mvinje pamoja na mteashuri, 1 ili kupapamba mahali pangu patakatifu, 2 nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu. 1
14Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako, 2 wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako, 1 nao watakuita Mji wa Bwana, 2 Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
15“Ingawa umeachwa na kuchukiwa, 2 bila yeyote anayesafiri ndani yako, 1 nitakufanya kuwa fahari ya milele, 2 na furaha ya vizazi vyote. 1
16Utanyonya maziwa ya mataifa, 2 na kunyonyeshwa matiti ya wafalme. 1 Ndipo utakapojua kwamba Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako, 2 Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo. 1
17Badala ya shaba nitakuletea dhahabu, 2 na fedha badala ya chuma. 1 Badala ya mti nitakuletea shaba, 2 na chuma badala ya mawe. 1 Nitafanya amani kuwa mtawala wako, 2 na haki kuwa mfalme wako. 1
18Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako, 2 wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako, 1 lakini utaita kuta zako Wokovu, 2 na malango yako Sifa. 1
19Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, 2 wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, 1 kwa maana Bwana atakuwa nuru yako ya milele, 2 naye Mungu wako atakuwa utukufu wako. 1
20Jua lako halitazama tena, 2 nao mwezi wako hautafifia tena; 1 Bwana atakuwa nuru yako milele, 2 nazo siku zako za huzuni zitakoma. 1
21Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu, 2 nao wataimiliki nchi milele. 1 Wao ni chipukizi nililolipanda, 2 kazi ya mikono yangu, 2 ili kuonyesha utukufu wangu. 1
22Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu, 2 mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu. 1 Mimi ndimi Bwana; 2 katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”