Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 51

1“Nisikilizeni, ninyi mnaofuatia haki 2 na mnaomtafuta Bwana: 1 Tazameni mwamba ambako mlichongwa, 2 na mahali pa kuvunjia mawe ambako mlichimbwa; 1

2mwangalieni Abrahamu, baba yenu, 2 na Sara, ambaye aliwazaa. 1 Wakati nilipomwita alikuwa mmoja tu, 2 nami nikambariki na kumfanya kuwa wengi. 1

3Hakika Bwana ataifariji Sayuni, 2 naye atayaangalia kwa huruma magofu yake yote; 1 atayafanya majangwa yake yawe kama Edeni, 2 nazo sehemu zake zisizolimika ziwe kama bustani ya Bwana. 1 Shangwe na furaha zitakuwako ndani yake, 2 shukrani na sauti za kuimba. 1

4“Nisikilizeni, watu wangu; 2 nisikieni, taifa langu: 1 Sheria itatoka kwangu; 2 haki yangu itakuwa nuru kwa mataifa. 1

5Haki yangu inakaribia mbio, 2 wokovu wangu unakuja, 2 nao mkono wangu utaleta hukumu kwa mataifa. 1 Visiwa vitanitegemea 2 na kungojea mkono wangu kwa matumaini. 1

6Inueni macho yenu mbinguni, 2 mkaitazame dunia chini; 1 mbingu zitatoweka kama moshi, 2 dunia itachakaa kama vazi, 2 na wakazi wake kufa kama mainzi. 1 Bali wokovu wangu utadumu milele, 2 haki yangu haitakoma kamwe. 1

7“Nisikieni, ninyi mnaojua lililo sawa, 2 ninyi watu ambao mna sheria yangu mioyoni mwenu: 1 Msiogope mashutumu ya wanadamu 2 wala msitiwe hofu na matukano yao. 1

8Kwa maana nondo atawala kama vazi, 2 nao funza atawatafuna kama sufu. 1 Lakini haki yangu itadumu milele, 2 wokovu wangu kwa vizazi vyote.” 1

9Amka, Amka! Jivike nguvu, 2 ewe mkono wa Bwana, 1 Amka, kama siku zilizopita, 2 kama vile vizazi vya zamani. 1 Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande, 2 uliyemchoma yule joka? 1

10Si ni wewe uliyekausha bahari, 2 maji ya kilindi kikuu, 1 uliyefanya barabara katika vilindi vya bahari 2 ili waliokombolewa wapate kuvuka? 1

11Wale waliolipiwa fidia na Bwana watarudi. 2 Wataingia Sayuni wakiimba; 2 furaha ya milele itakuwa taji juu ya vichwa vyao. 1 Furaha na shangwe zitawapata, 2 huzuni na kulia kwa uchungu kutatoweka. 1

12“Mimi, naam mimi, 2 ndimi niwafarijie ninyi. 1 Ninyi ni nani hata kuwaogopa 2 wanadamu wanaokufa, 2 wanadamu ambao ni majani tu, 1

13kwamba mnamsahau Bwana Muumba wenu, 2 aliyezitanda mbingu 2 na kuiweka misingi ya dunia, 1 kwamba mnaishi katika hofu siku zote 2 kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu, 2 ambaye nia yake ni kuangamiza? 1 Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu? 2

14Wafungwa waliojikunyata kwa hofu 2 watawekwa huru karibuni; 1 hawatafia kwenye gereza lao, 2 wala hawatakosa chakula. 1

15Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, 2 ambaye huisukasuka bahari ili mawimbi yake yangurume: 2 Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. 1

16Nimeweka maneno yangu kinywani mwako 2 na kukufunika kwa uvuli wa mkono wangu: 1 Mimi niliyeweka mbingu mahali pake, 2 niliyeweka misingi ya dunia, 1 niwaambiaye Sayuni, 2 ‘Ninyi ni watu wangu.’ ” 1 Kikombe Cha Ghadhabu Ya Bwana 1

17Amka, amka! 2 Simama, ee Yerusalemu, 1 wewe uliyekunywa kutoka mkono wa Bwana 2 kikombe cha ghadhabu yake, 1 wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake, 2 kikombe kile cha kunywea 2 kiwafanyacho watu kuyumbayumba. 1

18Kati ya wana wote aliowazaa 2 hakuwepo hata mmoja wa kumwongoza, 1 kati ya wana wote aliowalea 2 hakuwepo hata mmoja wa kumshika mkono. 1

19Majanga haya mawili yamekuja juu yako: 2 ni nani awezaye kukufariji? 1 Maangamizi, uharibifu, njaa na upanga: 2 ni nani awezaye kukutuliza? 1

20Wana wako wamezimia, 2 wamelala kwenye mwanzo wa kila barabara, 2 kama swala aliyenaswa kwenye wavu. 1 Wamejazwa na ghadhabu ya Bwana 2 na makaripio ya Mungu wako. 1

21Kwa hiyo sikiliza hili, wewe uliyeteswa, 2 uliyelewa, lakini si kwa mvinyo. 1

22Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi wako, 2 Mungu wako, yeye ambaye huwatetea watu wake: 1 “Tazama, nimeondoa mkononi mwako 2 kikombe kilichokufanya uyumbayumbe; 1 kutoka kikombe hicho, 2 kikombe cha kunywa cha ghadhabu yangu, 2 kamwe hutakunywa tena. 1

23Nitakiweka mikononi mwa watesi wako, 2 wale waliokuambia, 1 ‘Anguka kifudifudi 2 ili tuweze kutembea juu yako.’ 1 Ukaufanya mgongo wako kama ardhi, 2 kama njia yao ya kupita.”

← Isaiah 50Read In The App, Free →Isaiah 52 →

Study Isaiah 51

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566