Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 64

1Laiti ungelipasua mbingu na kushuka chini, 2 ili milima ingelitetemeka mbele zako! 1

2Kama vile moto uteketezavyo vijiti 2 na kusababisha maji kuchemka, 1 shuka ukafanye jina lako lijulikane kwa adui zako, 2 na kusababisha mataifa yatetemeke mbele zako! 1

3Kwa maana ulipofanya mambo ya kutisha ambayo hatukuyatazamia, 2 ulishuka, nayo milima ikatetemeka mbele zako. 1

4Tangu nyakati za zamani hakuna yeyote aliyesikia, 2 hakuna sikio lililotambua, 1 hakuna jicho lililomwona Mungu mwingine ila wewe, 2 anayetenda mambo kwa ajili ya wale wamngojeao. 1

5Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha, 2 wale wazikumbukao njia zako. 1 Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako, 2 ulikasirika. 2 Tutawezaje basi kuokolewa? 1

6Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi, 2 nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu; 1 sisi sote tunasinyaa kama jani, 2 na kama upepo maovu yetu hutupeperusha. 1

7Hakuna yeyote anayeliitia jina lako 2 wala anayejitahidi kukushika, 1 kwa kuwa umetuficha uso wako 2 na kutuacha tudhoofike kwa sababu ya dhambi zetu. 1

8Lakini, Ee Bwana, wewe ndiwe Baba yetu. 2 Sisi ni udongo, wewe ndiye mfinyanzi; 2 sisi sote tu kazi ya mkono wako. 1

9Ee Bwana, usikasirike kupita kiasi, 2 usizikumbuke dhambi zetu milele. 1 Ee Bwana, utuangalie, twakuomba, 2 kwa kuwa sisi sote tu watu wako. 1

10Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa; 2 hata Sayuni ni jangwa, Yerusalemu ni ukiwa. 1

11Hekalu letu takatifu na tukufu, mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe, 2 limechomwa kwa moto, 2 navyo vitu vyote tulivyovithamini vimeharibika. 1

12Ee Bwana, baada ya haya yote, utajizuia? 2 Je, utanyamaza kimya na kutuadhibu kupita kiasi?

← Isaiah 63Read In The App, Free →Isaiah 65 →

Study Isaiah 64

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566