Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 32

1Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu 2 na watawala watatawala kwa haki. 1

2Kila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo 2 na kimbilio kutokana na dhoruba, 1 kama vijito vya maji jangwani 2 na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu. 1

3Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena, 2 nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza. 1

4Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa, 2 nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha. 1

5Mpumbavu hataitwa tena muungwana, 2 wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu. 1

6Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, 2 moyo wake hushughulika na uovu: 1 Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu, 2 na hueneza habari za makosa kuhusu Bwana; 1 yeye huwaacha wenye njaa bila kitu, 2 na wenye kiu huwanyima maji. 1

7Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu, 2 hufanya mipango miovu 1 ili kumwangamiza maskini kwa uongo, 2 hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki. 1

8Lakini mtu muungwana hufanya mipango ya kiungwana, 2 na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa. 1 Wanawake Wa Yerusalemu 1

9Enyi wanawake wenye kuridhika sana, 2 amkeni na mnisikilize. 1 Enyi binti mnaojisikia kuwa salama, 2 sikieni lile ninalotaka kuwaambia! 1

10Muda zaidi kidogo ya mwaka mmoja, 2 ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka, 1 mavuno ya zabibu yatakoma 2 na mavuno ya matunda hayatakuwepo. 1

11Tetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika, 2 tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama! 1 Vueni nguo zenu, 2 vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu. 1

12Pigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri, 2 kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri 1

13na kwa ajili ya nchi ya watu wangu, 2 nchi ambayo miiba na michongoma imemea: 1 naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha 2 na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe. 1

14Ngome itaachwa, 2 mji wenye kelele nyingi utahamwa, 1 ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele, 2 mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo, 1

15mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu, 2 nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba, 2 na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu. 1

16Haki itakaa katika jangwa, 2 na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba. 1

17Matunda ya haki yatakuwa amani, 2 matokeo ya haki yatakuwa utulivu 2 na matumaini milele. 1

18Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani, 2 katika nyumba zilizo salama, 2 katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu. 1

19Hata kama mvua ya mawe iangushe msitu 2 na mji ubomolewe kabisa, 1

20tazama jinsi utakavyobarikiwa, 2 ukipanda mbegu yako katika kila kijito, 1 na kuwaacha ngʼombe wako 2 na punda wajilishe kwa uhuru.

← Isaiah 31Read In The App, Free →Isaiah 33 →

Study Isaiah 32

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566