Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 17

1Neno kuhusu Dameski: 1 “Tazama, Dameski haitakuwa tena mji 2 bali itakuwa lundo la magofu. 1

2Miji ya Aroeri itaachwa 2 na itaachiwa mifugo ambayo italala huko, 2 bila yeyote wa kuyaogopesha. 1

3Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu, 2 nao uweza wa ufalme kutoka Dameski; 1 mabaki ya Aramu yatakuwa 2 kama utukufu wa Waisraeli,” 4 asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 1

4“Katika siku ile utukufu wa Yakobo utafifia, 2 unono wa mwili wake utadhoofika. 1

5Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka 2 na kuvuna nafaka kwa mikono yake, 1 kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke 2 katika Bonde la Warefai. 1

6Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki, 2 kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa, 1 kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni, 2 nne au tano katika matawi yazaayo sana,” 4 asema Bwana, Mungu wa Israeli. 1

7Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao, 2 na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1

8Hawataziangalia tena madhabahu, 2 kazi za mikono yao, 1 nao hawataheshimu nguzo za Ashera, + 17:8 Ashera hapa maana yake ni mungu mke aliyekuwa akiabudiwa pamoja na Baali. 2 na madhabahu za kufukizia uvumba zilizofanywa kwa mikono yao.

9Katika siku ile miji yao iliyo imara, ambayo waliihama kwa sababu ya Waisraeli, itakuwa kama mahali palipoachwa pa vichaka na magugu. Nayo yote itakuwa ukiwa. 1

10Mmemsahau Mungu Mwokozi wenu, 2 hamkumkumbuka Mwamba aliye ngome yenu. 1 Kwa hiyo, hata ingawa mlipandikiza mimea iliyo mizuri sana 2 na kuotesha mizabibu ya kigeni, 1

11hata kama siku ile unapoipandikiza, unaifanya iote 2 na asubuhi ile ile unayoipanda, unaifanya ichipue, 1 hata hivyo mavuno yatakuwa kama si kitu 2 katika siku ile ya ugonjwa na maumivu yasiyoponyeka. 1

12Lo! Ghadhabu ya mataifa mengi, 2 wanaghadhibika kama bahari iliyochafuka! 1 Lo! Makelele ya mataifa 2 wanavuma kama ngurumo za maji mengi! 1

13Ingawa mataifa yanavuma kama ngurumo za maji yanayofanya mawimbi, 2 wakati anapoyakemea yanakimbia mbali, 1 yanafukuzwa mbele ya upepo kama makapi juu ya milima, 2 kama jani livingirishwapo na dhoruba. 1

14Wakati wa jioni, hofu ya ghafula! 2 Kabla ya asubuhi, wametoweka! 1 Hili ndilo fungu la wale wanaotupora, 2 fungu la wale wanaotunyangʼanya mali zetu.

← Isaiah 16Read In The App, Free →Isaiah 18 →

Study Isaiah 17

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566