Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 41

1“Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa! 2 Mataifa na wafanye upya nguvu zao! 1 Wao na wajitokeze, kisha waseme, 2 tukutane pamoja mahali pa hukumu. 1

2“Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki, 2 akimwita katika haki kwa utumishi wake? 1 Huyatia mataifa mikononi mwake, 2 na kuwatiisha wafalme mbele zake. 1 Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake, 2 huwafanya makapi yapeperushwayo na upepo kwa upinde wake. 1

3Huwafuatia na kuendelea salama, 2 katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita. 1

4Ni nani aliyefanya jambo hili na kulitimiliza, 2 akiita vizazi tangu mwanzo? 1 Mimi, Bwana, ni wa kwanza 2 nami nitakuwa pamoja na wa mwisho: 2 mimi Bwana ndiye.” 1

5Visiwa vimeliona na kuogopa, 2 miisho ya dunia inatetemeka. 1 Wanakaribia na kuja mbele, 2

6kila mmoja humsaidia mwingine 2 na kusema kwa ndugu yake, “Uwe hodari!” 1

7Fundi humtia moyo sonara, 2 yeye alainishaye kwa nyundo 2 humhimiza yeye agongeaye kwenye fuawe, 1 Humwambia yeye aunganishaye, “Ni kazi njema.” 2 Naye huikaza sanamu kwa misumari ili isitikisike. 1

8“Lakini wewe, ee Israeli, mtumishi wangu, 2 Yakobo, niliyemchagua, 2 ninyi wazao wa Abrahamu rafiki yangu, 1

9nilikuchukua toka miisho ya dunia, 2 nilikuita kutoka pembe zake za mbali. 1 Nilisema, ‘Wewe ni mtumishi wangu’; 2 nimekuchagua, wala sikukukataa. 1

10Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe; 2 usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. 1 Nitakutia nguvu na kukusaidia; 2 nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu. 1

11“Wote walioona hasira dhidi yako 2 hakika wataaibika na kutahayarika, 1 wale wakupingao 2 watakuwa kama vile si kitu, na kuangamia. 1

12Ingawa utawatafuta adui zako, 2 hutawaona. 1 Wale wanaopigana vita dhidi yako 2 watakuwa kama vile si kitu kabisa. 1

13Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, 2 nikushikaye mkono wako wa kuume 1 na kukuambia, Usiwe na hofu, 2 nitakusaidia. 1

14Usiogope, ee Yakobo uliye mdudu, 2 ee Israeli uliye mdogo, 1 kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia,” asema Bwana, 2 Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1

15“Tazama, nitakufanya chombo cha kupuria, 2 kipya na chenye makali, chenye meno mengi. 1 Utaipura milima na kuiponda 2 na kuvifanya vilima kuwa kama makapi. 1

16Utaipepeta, nao upepo utaichukua, 2 dhoruba itaipeperushia mbali. 1 Bali wewe utajifurahisha katika Bwana 2 na katika utukufu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1

17“Maskini na wahitaji wanatafuta maji, 2 lakini hayapo, 2 ndimi zao zimekauka kwa kiu. 1 Lakini Mimi Bwana nitawajibu, 2 Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha. 1

18Nitaifanya mito itiririke juu ya vilima vilivyo kame, 2 nazo chemchemi ndani ya mabonde. 1 Nitaligeuza jangwa liwe mabwawa ya maji, 2 nayo ardhi iliyokauka kuwa chemchemi za maji. 1

19Katika jangwa nitaotesha 2 mwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni. 1 Nitaweka misunobari, mivinje na misanduku 2 pamoja huko nyikani, 1

20ili kwamba watu wapate kuona na kujua, 2 wapate kufikiri na kuelewa, 1 kwamba mkono wa Bwana umetenda hili, 2 kwamba yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ndiye alilifanya.” 1

21Bwana asema, “Leta shauri lako. 2 Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo. 1

22“Leteni sanamu zenu zituambie 2 ni nini kitakachotokea. 1 Tuambieni mambo ya zamani yalikuwa nini, 2 ili tupate kuyatafakari 2 na kujua matokeo yake ya mwisho. 1 Au tutangazieni mambo yatakayokuja, 2

23tuambieni ni nini kitakachotokea baadaye, 2 ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu. 1 Fanyeni jambo lolote zuri au baya, 2 ili tupate kutishika na kujazwa na hofu. 1

24Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa, 2 na kazi zenu hazifai kitu kabisa; 2 yeye awachaguaye ni chukizo sana. 1

25“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini, 2 naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu. 1 Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope, 2 kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia. 1

26Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua, 2 au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’? 1 Hakuna aliyenena hili, 2 hakuna aliyetangulia kusema hili, 2 hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu. 1

27Nilikuwa wa kwanza kumwambia Sayuni, 2 ‘Tazama, wako hapa!’ 2 Nilimpa Yerusalemu mjumbe wa habari njema. 1

28Ninatazama, lakini hakuna yeyote: 2 hakuna yeyote miongoni mwao awezaye kutoa shauri, 2 hakuna yeyote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza. 1

29Tazama, wote ni ubatili! 2 Matendo yao ni bure; 2 vinyago vyao ni upepo mtupu na machafuko.

← Isaiah 40Read In The App, Free →Isaiah 42 →

Study Isaiah 41

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566