Isaiah 5
1Nitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye, 2 kuhusu shamba lake la mizabibu: 1 Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu 2 kwenye kilima chenye rutuba. 1
2Alililima na kuondoa mawe 2 na akaliotesha mizabibu bora sana. 1 Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake, 2 na kutengeneza shinikizo la kukamulia divai pia. 1 Kisha akatazamia kupata mazao ya zabibu nzuri, 2 lakini lilizaa matunda mabaya tu. 1
3“Basi enyi wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda, 2 hukumuni kati yangu na shamba langu la mizabibu. 1
4Ni nini zaidi ambacho kingeweza kufanyika kwa shamba langu la mizabibu 2 kuliko yale niliyofanya? 1 Nilipotazamia kupata zabibu nzuri, 2 kwa nini lilizaa zabibu mbaya tu? 1
5Sasa nitawaambia lile nitakalolitendea 2 shamba langu la mizabibu: 1 Nitaondoa uzio wake, 2 nalo litaharibiwa, 1 nitabomoa ukuta wake, 2 nalo litakanyagwa. 1
6Nitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu, 2 halitakatiwa matawi wala kulimwa, 1 nayo michongoma na miiba itamea huko, 2 nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.” 1
7Shamba la mzabibu la Bwana Mwenye Nguvu Zote 2 ni nyumba ya Israeli, 1 na watu wa Yuda 2 ni bustani yake ya kumpendeza. 1 Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu, 2 alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu. 1 Ole Na Hukumu 1
8Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba 2 na kuunganisha mashamba baada ya mashamba 1 hadi hakuna nafasi iliyobaki, 2 nanyi mnaishi peke yenu katika nchi. 1
9Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia: 2 “Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa, 2 nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa. 1
10Shamba la mizabibu la eka kumi 2 litatoa bathi + 5:10 Bathi moja ni sawa na lita 22. moja ya divai, 1 na homeri + 5:10 Homeri moja ni sawa na lita 220. ya mbegu zilizopandwa 2 itatoa efa + 5:10 Efa moja ni sawa na lita 22. moja tu ya nafaka.” 1
11Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema 2 wakikimbilia kunywa vileo, 1 wale wakawiao sana mpaka usiku, 2 mpaka wamewaka kwa mvinyo. 1
12Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao, 2 matari, filimbi na mvinyo, 1 lakini hawayajali matendo ya Bwana, 2 wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake. 1
13Kwa hiyo watu wangu watakwenda uhamishoni 2 kwa sababu ya kukosa ufahamu, 1 watu wao wenye vyeo watakufa kwa njaa 2 na watu wao wengi watakauka kwa kiu. 1
14Kwa hiyo kaburi + 5:14 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. limeongeza hamu yake 2 na kupanua mdomo wake bila kikomo, 1 ndani mwake watashuka wakuu wao na wingi wa watu, 2 pamoja na wagomvi wao, na wafanyao sherehe wote. 1
15Hivyo mwanadamu atashushwa, 2 na binadamu kunyenyekezwa, 2 macho ya wenye majivuno yatanyenyekezwa. 1
16Lakini Bwana Mwenye Nguvu Zote atatukuzwa 2 kwa ajili ya haki yake, 1 naye Mungu Mtakatifu atajionyesha mwenyewe 2 kuwa mtakatifu kwa haki yake. 1
17Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe, 2 wana-kondoo watajilisha katika magofu ya matajiri. 1
18Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifu 2 na uovu kama kwa kamba za mkokoteni, 1
19kwa wale wanaosema, “Mungu na afanye haraka, 2 aharakishe kazi yake ili tupate kuiona. 1 Huo mpango wa Aliye Mtakatifu wa Israeli na ukamilike, 2 tena udhihirike ili tupate kuujua.” 1
20Ole wao wanaoita ubaya ni wema, 2 na wema ni ubaya, 1 wawekao giza badala ya nuru, 2 na nuru badala ya giza, 1 wawekao uchungu badala ya utamu, 2 na utamu badala ya uchungu. 1
21Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe, 2 na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. 1
22Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo, 2 nao walio hodari katika kuchanganya vileo, 1
23wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo, 2 lakini huwanyima haki wasio na hatia. 1
24Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi, 2 na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, 1 ndivyo mizizi yao itakavyooza 2 na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; 1 kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote 2 na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
25Kwa hiyo hasira ya Bwana inawaka dhidi ya watu wake, 2 mkono wake umeinuliwa na anawapiga. 1 Milima inatetemeka, 2 maiti ni kama takataka kwenye barabara. 1 Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, 2 mkono wake bado umeinuliwa juu. 1
26Yeye anainua bendera kwa ajili ya mataifa yaliyo mbali, 2 anapiga filimbi kwa ajili ya wale walio kwenye miisho ya dunia. 1 Tazama wamekuja, 2 kwa kasi na kwa haraka! 1
27Hakuna hata mmoja wao anayechoka wala kujikwaa, 2 hakuna hata mmoja anayesinzia wala kulala, 1 hakuna mkanda uliolegezwa kiunoni, 2 hakuna gidamu ya kiatu iliyokatika. 1
28Mishale yao ni mikali, 2 pinde zao zote zimevutwa, 1 kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume, 2 magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli. 1
29Ngurumo yao ni kama ile ya simba, 2 wananguruma kama wana simba, 1 wanakoroma wanapokamata mawindo yao, 2 na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa. 1
30Katika siku ile watanguruma juu yake 2 kama ngurumo za bahari. 1 Kama mtu akiitazama nchi, 2 ataona giza na dhiki; 2 hata nuru itatiwa giza kwa mawingu.