Isaiah 40
1Wafarijini, wafarijini watu wangu, 2 asema Mungu wenu. 1
2Sema na Yerusalemu kwa upole, 2 umtangazie 1 kwamba kazi yake ngumu imekamilika, 2 kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia, 1 kwamba amepokea kutoka mkononi mwa Bwana 2 maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote. 1
3Sauti ya mtu aliaye: 2 “Itengenezeni jangwani njia ya Bwana, 1 nyoosheni njia kuu nyikani 2 kwa ajili ya Mungu wetu. 1
4Kila bonde litainuliwa, 2 kila mlima na kilima kitashushwa; 1 penye mabonde patanyooshwa, 2 napo palipoparuza patasawazishwa. 1
5Utukufu wa Bwana utafunuliwa, 2 nao wanadamu wote watauona pamoja. 4 Kwa maana kinywa cha Bwana kimenena.” 1
6Sauti husema, “Piga kelele.” 2 Nami nikasema, “Nipige kelele gani?” 1 “Wanadamu wote ni kama majani, 2 nao utukufu wao wote 2 ni kama maua ya kondeni. 1
7Majani hunyauka na maua huanguka, 2 kwa sababu pumzi ya Bwana huyapuliza. 2 Hakika wanadamu ni majani. 1
8Majani hunyauka na maua huanguka, 2 lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.” 1
9Wewe uletaye habari njema Sayuni, 2 panda juu ya mlima mrefu. 1 Wewe uletaye habari njema Yerusalemu, 2 inua sauti yako kwa kupiga kelele, 2 inua sauti, usiogope; 1 iambie miji ya Yuda, 2 “Yuko hapa Mungu wenu!” 1
10Tazameni, Bwana Mwenyezi anakuja na nguvu, 2 nao mkono wake ndio utawalao kwa ajili yake. 1 Tazameni, ujira wake u pamoja naye, 2 nayo malipo yake yanafuatana naye. 1
11Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo: 2 Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake 1 na kuwachukua karibu na moyo wake, 2 huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao. 1
12Ni nani aliyepima maji ya bahari 2 kwenye konzi ya mkono wake, 2 au kuzipima mbingu kwa shibiri + 40:12 Shibiri ni sawa na sentimita 20 au inchi 8. yake? 1 Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu, 2 au kupima milima kwenye kipimio 2 na vilima kwenye mizani? 1
13Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana, 2 au kumfundisha akiwa kama mshauri wake? 1
14Ni nani ambaye Bwana ametaka shauri kwake ili kumwelimisha, 2 naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa? 1 Ni nani aliyemfundisha maarifa 2 au kumwonyesha mapito ya ufahamu? 1
15Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo, 2 ni kama vumbi jembamba juu ya mizani, 2 huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini. 1
16Lebanoni hautoshi kwa moto wa madhabahuni, 2 wala wanyama wake hawatoshi kwa sadaka za kuteketezwa. 1
17Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu, 2 yanaonekana yasio na thamani 2 na zaidi ya bure kabisa. 1
18Basi, utamlinganisha Mungu na nani? 2 Utamlinganisha na kitu gani? 1
19Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu, 2 naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu 2 na kuitengenezea mikufu ya fedha. 1
20Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii 2 huuchagua mti usiooza. 1 Humtafuta fundi stadi 2 wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika. 1
21Je, hujui? 2 Je, hujasikia? 1 Je, hujaambiwa tangu mwanzo? 2 Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia? 1
22Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia, 2 nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi. 1 Huzitandaza mbingu kama chandarua, 2 na kuzitandaza kama hema la kuishi. 1
23Huwafanya wakuu kuwa si kitu, 2 na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure. 1
24Mara baada ya kupandwa, 2 mara baada ya kutiwa ardhini, 2 mara baada ya kutoa mizizi yao ardhini, 1 ndipo huwapulizia nao wakanyauka, 2 nao upepo wa kisulisuli 2 huwapeperusha kama makapi. 1
25“Utanilinganisha mimi na nani? 2 Au ni nani anayelingana nami?” asema yeye Aliye Mtakatifu. 1
26Inueni macho yenu mtazame mbinguni: 2 Ni nani aliyeumba hivi vyote? 1 Ni yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine 2 na kuziita kila moja kwa jina lake. 1 Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu, 2 hakuna hata mojawapo inayokosekana. 1
27Kwa nini unasema, ee Yakobo, 2 nanyi ee Israeli, kulalamika, 1 “Njia yangu imefichwa Bwana asiione, 2 Mungu wangu hajali shauri langu?” 1
28Je wewe, hufahamu? 2 Je wewe, hujasikia? 1 Bwana ni Mungu wa milele, 2 Muumba wa miisho ya dunia. 1 Hatachoka wala kulegea, 2 wala hakuna hata mmoja 2 awezaye kuupima ufahamu wake. 1
29Huwapa nguvu waliolegea 2 na huongeza nguvu za wadhaifu. 1
30Hata vijana huchoka na kulegea, 2 nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka, 1
31bali wale wamtumainio Bwana 2 atafanya upya nguvu zao. 1 Watapaa juu kwa mbawa kama tai; 2 watapiga mbio wala hawatachoka, 2 watatembea kwa miguu wala hawatazimia.