Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 18

1Ole kwa nchi ya mvumo wa mabawa, + 18:1 Au: wa nzige. 2 kando ya mito ya Kushi, 1

2iwapelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari 2 kwa mashua za mafunjo juu ya maji. 1 Nendeni, wajumbe wepesi, 2 kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, 2 kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, 1 taifa gomvi lenye lugha ngeni, 2 ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito. 1

3Enyi mataifa yote ya ulimwengu, 2 ninyi mnaoishi duniani 1 wakati bendera itakapoinuliwa milimani, 2 mtaiona, 1 nayo tarumbeta itakapolia, 2 mtaisikia. 1

4Hili ndilo Bwana aliloniambia: 2 “Nitatulia kimya na kutazama 2 kutoka maskani yangu, 1 kama joto linalometameta katika mwanga wa jua, 2 kama wingu la umande 2 katika joto la wakati wa mavuno.” 1

5Kwa maana, kabla ya mavuno, 2 wakati wa kuchanua ukishapita 2 na maua yakawa zabibu zinazoiva, 1 atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi, 2 naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka. 1

6Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimani 2 na wanyama pori, 1 ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi, 2 nao wanyama pori wakati wote wa masika.

7Wakati huo matoleo yataletwa kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote 1 kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, 2 kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, 1 kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni, 2 ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito, matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote.

← Isaiah 17Read In The App, Free →Isaiah 19 →

Study Isaiah 18

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566