Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 33

1Ole wako wewe, ee mharabu, 2 wewe ambaye hukuharibiwa! 1 Ole wako, ee msaliti, 2 wewe ambaye hukusalitiwa! 1 Utakapokwisha kuharibu, 2 utaharibiwa; 1 utakapokwisha kusaliti, 2 utasalitiwa. 1

2Ee Bwana, uturehemu, 2 tunakutamani. 1 Uwe nguvu yetu kila asubuhi 2 na wokovu wetu wakati wa taabu. 1

3Kwa ngurumo ya sauti yako, mataifa yanakimbia; 2 unapoinuka, mataifa hutawanyika. 1

4Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu, 2 kama kundi la nzige watu huvamia juu yake. 1

5Bwana ametukuka, kwa kuwa anakaa mahali palipoinuka, 2 ataijaza Sayuni kwa haki na uadilifu. 1

6Atakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu, 2 ghala za wokovu tele, hekima na maarifa; 2 kumcha Bwana ni ufunguo wa hazina hii. 1

7Angalia, watu wake mashujaa wanapiga kelele kwa nguvu barabarani, 2 wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu. 1

8Njia kuu zimeachwa, 2 hakuna wasafiri barabarani. 1 Mkataba umevunjika, 2 mashahidi wake wamedharauliwa, + 33:8 Au: miji yake imedharauliwa. 2 hakuna yeyote anayeheshimiwa. 1

9Ardhi inaomboleza + 33:9 Au: Ardhi inakauka. na kuchakaa, 2 Lebanoni imeaibika na kunyauka, 1 Sharoni ni kama Araba, 2 nayo Bashani na Karmeli 2 wanapukutisha majani yao. 1

10“Sasa nitainuka,” asema Bwana. 2 “Sasa nitatukuzwa; 2 sasa nitainuliwa juu. 1

11Mlichukua mimba ya makapi, 2 mkazaa mabua, 2 pumzi yenu ni moto uwateketezao. 1

12Mataifa yatachomwa kama ichomwavyo chokaa, 2 kama vichaka vya miiba vilivyokatwa ndivyo watakavyochomwa.” 1

13Ninyi mlio mbali sana, sikieni lile nililofanya; 2 ninyi mlio karibu, tambueni uweza wangu! 1

14Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu, 2 kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu: 1 “Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao? 2 Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?” 1

15Yeye aendaye kwa uadilifu 2 na kusema lililo haki, 1 yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma 2 na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, 1 yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji, 2 na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu: 1

16huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu, 2 ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani. 1 Atapewa mkate wake, 2 na maji yake hayatakoma. 1

17Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake 2 na kuiona nchi inayoenea mbali. 1

18Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita: 2 “Yuko wapi yule afisa mkuu? 2 Yuko wapi yule aliyechukua ushuru? 2 Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?” 1

19Hutawaona tena wale watu wenye kiburi, 2 wale watu wenye usemi wa mafumbo, 2 wenye lugha ngeni, isiyoeleweka. 1

20Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu; 2 macho yenu yatauona Yerusalemu, 2 mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa, 1 nguzo zake hazitangʼolewa kamwe, 2 wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika. 1

21Huko Bwana atakuwa Mwenye Nguvu wetu. 2 Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito. 1 Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko, 2 wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko. 1

22Kwa kuwa Bwana ni mwamuzi wetu, 2 Bwana ndiye mtoa sheria wetu, 1 Bwana ni mfalme wetu, 2 yeye ndiye atakayetuokoa. 1

23Kamba zenu za merikebu zimelegea: 2 Mlingoti haukusimama imara, 2 nalo tanga halikukunjuliwa. 1 Wingi wa mateka yatagawanywa, 2 hata yeye aliye mlemavu atachukua nyara. 1

24Hakuna yeyote aishiye Sayuni atakayesema, “Mimi ni mgonjwa”; 2 nazo dhambi za wale waishio humo zitasamehewa.

← Isaiah 32Read In The App, Free →Isaiah 34 →

Study Isaiah 33

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566