Isaiah 14
1Bwana atamhurumia Yakobo, 2 atamchagua Israeli tena, 2 na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe. 1 Wageni wataungana nao 2 na kujiunga na nyumba ya Yakobo. 1
2Mataifa watawachukua 2 na kuwaleta mahali pao wenyewe. 1 Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa 2 kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana. 1 Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, 2 na kutawala juu ya wale waliowaonea.
3Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili,
4utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli: 1 Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho! 2 Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma! 1
5Bwana amevunja fimbo ya mwovu, 2 fimbo ya utawala ya watawala, 1
6ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa 2 kwa mapigo yasiyo na kikomo, 1 nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa 2 kwa jeuri pasipo huruma. 1
7Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani, 2 wanabubujika kwa kuimba. 1
8Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni 2 inashangilia mbele yako na kusema, 1 “Basi kwa sababu umeangushwa chini, 2 hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.” 1
9Kuzimu kote kumetaharuki 2 kukulaki unapokuja, 1 kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, 2 wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, 1 kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme: 2 wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa. 1
10Wote wataitikia, 2 watakuambia, 1 “Wewe pia umekuwa dhaifu, kama sisi tulivyo; 2 wewe umekuwa kama sisi.” 1
11Majivuno yako yote yameshushwa mpaka kuzimu, 2 pamoja na kelele ya vinubi vyako, 1 mafunza yametanda chini yako, 2 na minyoo imekufunika. 1
12Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, 2 ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko! 1 Umetupwa chini duniani, 2 wewe uliyepata kuangusha mataifa! 1
13Ulisema moyoni mwako, 2 “Nitapanda juu hadi mbinguni, 1 nitakiinua kiti changu cha enzi 2 juu ya nyota za Mungu, 1 nitaketi nimetawazwa 2 juu ya mlima wa kusanyiko, 2 kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu. 1
14Nitapaa juu kupita mawingu, 2 nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.” 1
15Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu, 2 hadi kwenye vina vya shimo. 1
16Wale wanaokuona wanakukazia macho, 2 wanatafakari hatima yako: 1 “Je, huyu ndiye yule aliyetikisa dunia 2 na kufanya falme zitetemeke, 1
17yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa, 2 aliyeipindua miji yake, 1 na ambaye hakuwaachia mateka wake 2 waende nyumbani?” 1
18Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshima 2 kila mmoja katika kaburi lake. 1
19Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako 2 kama tawi lililokataliwa, 1 umefunikwa na waliouawa 2 pamoja na wale waliochomwa kwa upanga, 1 wale washukao mpaka 2 kwenye mawe ya shimo. 1 Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo, 2
20Hutajumuika nao kwenye mazishi, 1 kwa kuwa umeharibu nchi yako 2 na kuwaua watu wako. 1 Mzao wa mwovu 2 hatatajwa tena kamwe. 1
21Andaa mahali pa kuwachinjia wanawe 2 kwa ajili ya dhambi za baba zao, 1 wasije wakainuka ili kuirithi nchi 2 na kuijaza dunia kwa miji yao. 1
22Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, 2 “Nitainuka dhidi yao, 1 nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika, 2 watoto wake na wazao wake,” 4 asema Bwana. 1
23“Nitaifanya kuwa mahali pa bundi, 2 na kuwa nchi ya matope; 1 nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,” 2 asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 1 Unabii Dhidi Ya Ashuru
24Bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa, 1 “Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa, 2 nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama. 1
25Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu, 2 juu ya milima yangu nitawakanyagia chini. 1 Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu, 2 nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.” 1
26Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote, 2 huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote. 1
27Kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amekusudia, 2 ni nani awezaye kumzuia? 1 Mkono wake umenyooshwa, 2 ni nani awezaye kuurudisha? 1 Unabii Dhidi Ya Wafilisti
28Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki: 1
29Msifurahi, enyi Wafilisti wote, 2 kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika; 1 kutoka mzizi wa huyo nyoka 2 atachipuka nyoka mwenye sumu kali, 1 uzao wake utakuwa joka lirukalo, 2 lenye sumu kali. 1
30Maskini kuliko maskini wote watapata malisho, 2 nao wahitaji watalala salama. 1 Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa, 2 nayo njaa itawaua walionusurika. 1
31Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji! 2 Yeyukeni, enyi Wafilisti wote! 1 Wingu la moshi linakuja toka kaskazini, 2 wala hakuna atakayechelewa katika safu zake. 1
32Ni jibu gani litakalotolewa 2 kwa wajumbe wa taifa hilo? 1 “ Bwana ameifanya imara Sayuni, 2 nako ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”