Isaiah 47
1“Shuka uketi mavumbini, 2 ee Bikira Binti Babeli; 1 keti chini pasipo na kiti cha enzi, 2 ee binti wa Wakaldayo. 1 Hutaitwa tena mwororo wala wa kupendeza. 1
2Chukua mawe ya kusagia, usage unga, 2 vua shela yako. 1 Pandisha mavazi yako, ondoa viatu vyako, 2 vuka vijito kwa shida. 1
3Uchi wako utafunuliwa 2 na aibu yako itaonekana. 1 Nitalipa kisasi; 2 sitamhurumia hata mmoja.” 1
4Mkombozi wetu: Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake; 2 ndiye yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
5“Keti kimya, ingia gizani, 2 Binti wa Wakaldayo, 2 hutaitwa tena malkia wa falme. 1
6Niliwakasirikia watu wangu 2 na kuaibisha urithi wangu; 1 niliwatia mikononi mwako, 2 nawe hukuwaonea huruma. 1 Hata juu ya wazee 2 uliweka nira nzito sana. 1
7Ukasema, ‘Nitaendelea 2 kuwa malkia milele!’ 1 Lakini hukutafakari mambo haya 2 wala hukuwaza juu ya kile kingeweza kutokea. 1
8“Sasa basi, sikiliza, ewe kiumbe mpenda anasa, 2 ukaaye mahali pako pa salama, 1 na kujiambia mwenyewe, 2 ‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu. 1 Kamwe sitakuwa mjane, 2 wala sitafiwa na watoto.’ 1
9Haya mawili yatakupata, kufumba na kufumbua, 2 katika siku moja: 2 kufiwa na watoto, na ujane. 1 Yote yatakupata kwa kipimo kikamilifu, 2 ijapokuwa uchawi wako ni mwingi, 2 na uaguzi wako ni mwingi. 1
10Umeutegemea uovu wako, 2 nawe umesema, ‘Hakuna yeyote anionaye.’ 1 Hekima yako na maarifa yako vinakupoteza 2 unapojiambia mwenyewe, 2 ‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu.’ 1
11Maafa yatakujia, 2 nawe hutaweza kuyaondoa kwa uaguzi. 1 Janga litakuangukia, 2 wala hutaweza kulikinga kwa fidia; 1 msiba mkuu usioweza kuutabiri 2 utakujia ghafula. 1
12“Endelea basi na uaguzi wako, 2 na wingi wa uchawi wako, 2 ambao umeutumikia tangu utoto wako. 1 Labda utafanikiwa, 2 labda unaweza ukasababisha hofu kuu. 1
13Ushauri wote uliopokea umekuchosha bure! 2 Wanajimu wako na waje mbele, 1 wale watazama nyota watabiriao mwezi baada ya mwezi, 2 wao na wawaokoe na lile linalokuja juu yenu. 1
14Hakika wako kama mabua makavu; 2 moto utawateketeza. 1 Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe 2 kutokana na nguvu za mwali wa moto. 1 Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu yeyote joto; 2 hapa hakuna moto wa kuota. 1
15Hayo ndiyo yote wanayoweza kuwatendea ninyi, 2 hawa ambao umetaabika nao 2 na kufanya nao biashara tangu utoto. 1 Kila mmoja atatoroka; 2 hakuna yeyote awezaye kukuokoa.