Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 56

1Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Dumisheni haki 2 na mkatende lile lililo sawa, 1 kwa maana wokovu wangu u karibu 2 na haki yangu itafunuliwa upesi. 1

2Amebarikiwa mtu yule atendaye hili, 2 mtu yule alishikaye kwa uthabiti, 1 yeye ashikaye Sabato bila kuinajisi, 2 auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.” 1

3Usimwache mgeni aambatanaye na Bwana aseme, 2 “Hakika Bwana atanitenga na watu wake.” 1 Usimwache towashi yeyote alalamike akisema, 2 “Mimi ni mti mkavu tu.”

4Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kwa matowashi washikao Sabato zangu, 2 ambao huchagua kile kinachonipendeza 2 na kulishika sana agano langu: 1

5hao nitawapa ndani ya Hekalu langu na kuta zake 2 kumbukumbu na jina bora 2 kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike: 1 nitawapa jina lidumulo milele, 2 ambalo halitakatiliwa mbali. 1

6Wageni wanaoambatana na Bwana 2 ili kumtumikia, 1 kulipenda jina la Bwana, 2 na kumwabudu yeye, 1 wote washikao Sabato bila kuinajisi 2 na ambao hushika sana agano langu: 1

7hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu 2 na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala. 1 Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao 2 zitakubalika juu ya madhabahu yangu; 1 kwa maana nyumba yangu itaitwa 2 nyumba ya sala kwa mataifa yote.” 1

8Bwana Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye 2 Waisraeli waliohamishwa: 1 “Bado nitawakusanya wengine kwao 2 zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.” 1 Mashtaka Ya Mungu Dhidi Ya Waovu 1

9Njooni, enyi wanyama wote wa kondeni, 2 njooni mle, ninyi wanyama wote wa mwituni! 1

10Walinzi wa Israeli ni vipofu, 2 wote wamepungukiwa na maarifa; 1 wote ni mbwa walio bubu, 2 hawawezi kubweka; 1 hulala na kuota ndoto, 2 hupenda kulala. 1

11Ni mbwa wenye tamaa kubwa, 2 kamwe hawatosheki. 1 Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu; 2 wote wamegeukia njia yao wenyewe, 2 kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe. 1

12Kila mmoja hulia, “Njooni, tupate mvinyo! 2 Tunywe kileo sana! 1 Kesho itakuwa kama leo, 2 au hata bora zaidi.”

← Isaiah 55Read In The App, Free →Isaiah 57 →

Study Isaiah 56

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566