Isaiah 58
1“Piga kelele, usizuie. 2 Paza sauti yako kama tarumbeta. 1 Watangazieni watu wangu uasi wao, 2 na kwa nyumba ya Yakobo dhambi zao. 1
2Kwa maana kila siku hunitafuta, 2 wanaonekana kutaka kujua njia zangu, 1 kana kwamba walikuwa taifa linalotenda lililo sawa, 2 na ambalo halijaziacha amri za Mungu wake. 1 Hutaka kwangu maamuzi ya haki, 2 nao hutamani Mungu awakaribie. 1
3Wao husema, ‘Mbona tumefunga, nawe hujaona? 2 Mbona tumejinyenyekeza, nawe huangalii?’ 1 “Lakini katika siku ya kufunga kwenu, mnafanya mnavyotaka 2 na kuwadhulumu wafanyakazi wenu wote. 1
4Kufunga kwenu huishia kwenye magomvi na mapigano, 2 na kupigana ninyi kwa ninyi kwa ngumi za uovu. 1 Hamwezi kufunga kama mnavyofanya leo 2 na kutazamia sauti zenu kusikiwa huko juu. 1
5Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua, 2 siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza? 1 Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete, 2 na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu? 1 Je, huo ndio mnaouita mfungo, 2 siku iliyokubalika kwa Bwana? 1
6“Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua: 2 kufungua minyororo ya udhalimu, 2 na kufungua kamba za nira, 1 kuwaweka huru walioonewa, 2 na kuvunja kila nira? 1
7Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa 2 na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi, 1 unapomwona aliye uchi, umvike, 2 wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe? 1
8Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko 2 na uponyaji wako utatokea upesi; 1 ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako, 2 na utukufu wa Bwana utakuwa mlinzi nyuma yako. 1
9Ndipo utaita, naye Bwana atajibu, 2 utalia kuomba msaada, 2 naye atasema: Mimi hapa. 1 “Kama ukiiondoa nira ya udhalimu, 2 na kunyoosha kidole na kuzungumza maovu, 1
10nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu 2 na kutosheleza mahitaji ya walioonewa, 1 ndipo nuru yenu itakapongʼaa gizani, 2 nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri. 1
11Bwana atakuongoza siku zote, 2 atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame, 2 naye ataitia nguvu mifupa yako. 1 Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri, 2 kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe. 1
12Watu wako watajenga tena magofu ya zamani 2 na kuinua misingi ya kale; 1 utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka, 2 Mwenye Kurejeza Barabara za Makao. 1
13“Kama ukitunza miguu yako isivunje Sabato, 2 na kutokufanya kama vile upendavyo katika siku yangu takatifu, 1 kama ukiita Sabato siku ya furaha 2 na siku takatifu ya Bwana ya kuheshimiwa, 1 kama utaiheshimu kwa kutoenenda 2 katika njia zako mwenyewe, 1 na kutokufanya yakupendezayo 2 au kusema maneno ya upuzi, 1
14ndipo utakapojipatia furaha yako katika Bwana, 2 nami nitakufanya upande juu ya miinuko ya nchi 1 na kusherehekea urithi wa Yakobo baba yako.” 4 Kinywa cha Bwana kimenena haya.