Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 52

1Amka, amka, ee Sayuni, 2 jivike nguvu. 1 Vaa mavazi yako ya fahari, 2 ee Yerusalemu, mji mtakatifu. 1 Asiyetahiriwa na aliye najisi 2 hataingia kwako tena. 1

2Jikungʼute mavumbi yako, 2 inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu. 1 Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako, 2 ee Binti Sayuni uliye mateka.

3Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Mliuzwa pasipo malipo, 2 nanyi mtakombolewa bila fedha.”

4Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: 1 “Hapo kwanza watu wangu walishuka Misri kuishi, 2 hatimaye, Ashuru wakawaonea.

5“Basi sasa nina nini hapa?” asema Bwana. 1 “Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo, 2 nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,” 4 asema Bwana. 1 “Mchana kutwa 2 jina langu limetukanwa bila kikomo. 1

6Kwa hiyo watu wangu watalijua Jina langu; 2 kwa hiyo katika siku ile watajua 1 kwamba ndimi niliyetangulia kulisema. 2 Naam, ni mimi.” 1

7Tazama jinsi miguu ya wale waletao habari njema 2 ilivyo mizuri juu ya milima, 1 wale wanaotangaza amani, 2 wanaoleta habari njema, 2 wanaotangaza wokovu, 1 wauambiao Sayuni, 2 “Mungu wako anatawala!” 1

8Sikiliza! Walinzi wako wanapaza sauti zao, 2 pamoja wanapaza sauti zao kwa furaha. 1 Wakati Bwana atakaporejea Sayuni, 2 wataliona kwa macho yao wenyewe. 1

9Pazeni sauti ya nyimbo za furaha pamoja, 2 enyi magofu ya Yerusalemu, 1 kwa maana Bwana amewafariji watu wake, 2 ameikomboa Yerusalemu. 1

10Mkono mtakatifu wa Bwana umefunuliwa 2 machoni pa mataifa yote, 1 nayo miisho yote ya dunia itaona 2 wokovu wa Mungu wetu. 1

11Ondokeni, ondokeni, tokeni huko! 2 Msiguse kitu chochote kilicho najisi! 1 Tokeni kati yake mwe safi, 2 ninyi mchukuao vyombo vya Bwana. 1

12Lakini hamtaondoka kwa haraka, 2 wala hamtakwenda kwa kukimbia; 1 kwa maana Bwana atatangulia mbele yenu, 2 Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi nyuma yenu. 1 Mateso Na Utukufu Wa Mtumishi 1

13Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa hekima; 2 atatukuzwa, na kuinuliwa juu, na kukwezwa sana. 1

14Kama walivyokuwa wengi 2 walioshangazwa naye, 1 kwani uso wake ulikuwa umeharibiwa sana 2 zaidi ya mtu yeyote 1 na umbo lake kuharibiwa 2 zaidi ya mfano wa mwanadamu: 1

15hivyo atayashangaza mataifa mengi, 2 nao wafalme watafunga vinywa vyao kwa sababu yake. 1 Kwa kuwa yale ambayo hawakuambiwa, watayaona, 2 nayo yale wasiyoyasikia, watayafahamu.

← Isaiah 51Read In The App, Free →Isaiah 53 →

Study Isaiah 52

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566