Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 62

1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, 2 kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, 1 mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko, 2 wokovu wake kama mwanga wa moto. 1

2Mataifa wataona haki yako, 2 nao wafalme wote wataona utukufu wako; 1 wewe utaitwa kwa jina jipya 2 lile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka. 1

3Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana, 2 taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako. 1

4Hawatakuita tena Aliyeachwa, 2 wala nchi yako kuiita Ukiwa. 1 Bali utaitwa Hefsiba, + 62:4 Hefsiba maana yake Yeye ninayemfurahia. 2 nayo nchi yako itaitwa Beula, + 62:4 Beula maana yake Aliyeolewa. 1 kwa maana Bwana atakufurahia, 2 nayo nchi yako itaolewa. 1

5Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, 2 ndivyo wanao + 62:5 Au: wajenzi wako. watakavyokuoa wewe; 1 kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, 2 ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 1

6Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu, 2 hawatanyamaza mchana wala usiku. 1 Ninyi wenye kumwita Bwana, 2 msitulie, 1

7msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu 2 na kuufanya uwe sifa ya dunia. 1

8Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume 2 na kwa mkono wake wenye nguvu: 1 “Kamwe sitawapa tena adui zenu 2 nafaka zenu kama chakula chao; 1 kamwe wageni hawatakunywa tena 2 divai mpya ambayo mmeitaabikia, 1

9lakini wale waivunao nafaka wataila 2 na kumsifu Bwana, 1 nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake 2 katika nyua za patakatifu pangu.” 1

10Piteni, piteni katika malango! 2 Tengenezeni njia kwa ajili ya watu. 1 Jengeni, jengeni njia kuu! 2 Ondoeni mawe. 1 Inueni bendera kwa ajili ya mataifa. 1

11Bwana ametoa tangazo 2 mpaka miisho ya dunia: 1 “Mwambie Binti Sayuni, 2 ‘Tazama, mwokozi wako anakuja! 1 Tazama ujira wake uko pamoja naye, 2 na malipo yake yanafuatana naye!’ ” 1

12Wataitwa Watu Watakatifu, 2 Waliokombolewa na Bwana; 2 nawe utaitwa Aliyetafutwa, 2 Mji Usioachwa Tena.

← Isaiah 61Read In The App, Free →Isaiah 63 →

Study Isaiah 62

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566