Isaiah 43
1Lakini sasa hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye aliyekuumba, ee Yakobo, 2 yeye aliyekuhuluku, ee Israeli: 1 “Usiogope kwa maana nimekukomboa, 2 nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu. 1
2Unapopita kwenye maji makuu, 2 nitakuwa pamoja nawe, 1 unapopita katika mito ya maji, 2 hayatakugharikisha. 1 Utakapopita katika moto, 2 hutaungua, 2 miali ya moto haitakuunguza. 1
3Kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako. 1 Ninaitoa Misri kuwa fidia yako, 2 Kushi na Seba badala yako. 1
4Kwa kuwa wewe ni wa thamani na wa kuheshimiwa machoni pangu, 2 nami kwa kuwa ninakupenda, 1 nitatoa watu badala yako 2 na mataifa badala ya maisha yako. 1
5Usiogope, kwa kuwa mimi nipo pamoja nawe, 2 nitawaleta watoto wako kutoka mashariki, 2 na kukukusanya kutoka magharibi. 1
6Nitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’ 2 nayo kusini, ‘Usiwazuie.’ 1 Walete wana wangu kutoka mbali, 2 na binti zangu kutoka miisho ya dunia: 1
7kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu, 2 niliyemuumba kwa utukufu wangu, 2 niliyemhuluku na kumfanya.” 1
8Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni, 2 wenye masikio lakini hawasikii. 1
9Mataifa yote yanakutanika pamoja, 2 na makabila yanakusanyika. 1 Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya, 2 na kututangazia mambo yaliyopita? 1 Walete mashahidi wao ili kuwathibitisha kuwa walikuwa sahihi, 2 ili wengine waweze kusikia, waseme, “Ni kweli.” 1
10“Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana, 2 “na mtumishi wangu niliyemchagua, 1 ili mpate kunijua na kuniamini, 2 na kutambua kwamba Mimi ndiye. 1 Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa, 2 wala hatakuwepo mwingine baada yangu. 1
11Mimi, naam mimi, ndimi Bwana, 2 zaidi yangu hakuna mwokozi. 1
12Nimedhihirisha, kuokoa na kutangaza: 2 Mimi, wala si mungu mgeni katikati yenu. 1 Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana, 2 “kwamba Mimi ndimi Mungu. 2
13Naam, tangu siku za kale, Mimi ndiye. 1 Hakuna hata mmoja awezaye kuokoa 2 kutoka mkononi wangu. 1 Mimi ninapotenda, 2 ni nani awezaye kutangua?” 1 Huruma Za Mungu, Na Kukosa Uaminifu Kwa Israeli 1
14Hili ndilo Bwana asemalo, 2 Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: 1 “Kwa ajili yenu nitatumana Babeli 2 na kuwaleta Wakaldayo wote kama wakimbizi, 2 katika meli walizozionea fahari. 1
15Mimi ndimi Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wako, 2 Muumba wa Israeli, Mfalme wako.” 1
16Hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye aliyefanya njia baharini, 2 mahali pa kupita kwenye maji mengi, 1
17aliyeyakokota magari ya vita na farasi, 2 jeshi pamoja na askari wa msaada, 1 nao wakalala huko, wala hawatainuka tena kamwe, 2 wakakomeshwa, na wakazimika kama utambi: 1
18“Msiyakumbuke mambo yaliyopita, 2 wala msiyatafakari mambo ya zamani. 1
19Tazama, nitafanya jambo jipya! 2 Sasa litachipuka, je, hamtalitambua? 1 Nitafanya njia jangwani 2 na vijito vya maji katika nchi kame. 1
20Wanyama wa mwituni wataniheshimu, 2 mbweha na bundi, 1 kwa sababu ninawapatia maji jangwani, 2 na vijito katika nchi kame, 1 ili kuwapa watu wangu maji, wale niliowachagua, 2
21watu wale niliowaumba kwa ajili yangu, 2 ili wapate kutangaza sifa zangu. 1
22“Hata hivyo hukuniita mimi, ee Yakobo, 2 hujajitaabisha kwa ajili yangu, ee Israeli. 1
23Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, 2 wala kuniheshimu kwa dhabihu zako. 1 Sikukulemea kwa sadaka za nafaka 2 wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba. 1
24Hukuninunulia uvumba wowote wenye manukato, 2 wala hukunipa kwa ukarimu 2 mafuta ya wanyama wa dhabihu zako. 1 Lakini umenilemea kwa dhambi zako, 2 na kunitaabisha kwa makosa yako. 1
25“Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako, 2 kwa ajili yangu mwenyewe, 2 wala sizikumbuki dhambi zako tena. 1
26Tafakari mambo yaliyopita, 2 njoo na tuhojiane, 2 leta shauri lako uweze kupewa haki yako. 1
27Baba yako wa kwanza alitenda dhambi, 2 wasemaji wako wameasi dhidi yangu. 1
28Kwa hiyo nitawaaibisha wakuu wa Hekalu lako, 2 nami nitamtoa Yakobo aangamizwe, 2 na Israeli adhihakiwe.