Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 61

1Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu, 2 kwa sababu Bwana amenitia mafuta 2 kuwahubiria maskini habari njema. 1 Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, 2 kuwatangazia mateka uhuru wao, 1 na hao waliofungwa 2 habari za kufunguliwa kwao; 1

2kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, 2 na siku ya kisasi ya Mungu wetu, 1 kuwafariji wote waombolezao, 2

3na kuwapa mahitaji 2 wale wanaohuzunika katika Sayuni, 1 ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu, 2 mafuta ya furaha badala ya maombolezo, 2 vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa. 1 Nao wataitwa mialoni ya haki, 2 pando la Bwana, 2 ili kuonyesha utukufu wake. 1

4Watajenga upya magofu ya zamani 2 na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani; 1 watafanya upya miji iliyoharibiwa, 2 iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi. 1

5Wageni watayachunga makundi yenu, 2 wageni watafanya kazi katika mashamba yenu, 2 na kutunza mashamba yenu ya mizabibu. 1

6Nanyi mtaitwa makuhani wa Bwana, 2 mtaitwa watumishi wa Mungu wetu. 1 Mtakula utajiri wa mataifa, 2 nanyi katika utajiri wao mtajisifu. 1

7Badala ya aibu yao 2 watu wangu watapokea sehemu maradufu, 1 na badala ya fedheha 2 watafurahia katika urithi wao; 1 hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao, 2 nayo furaha ya milele itakuwa yao. 1

8“Kwa maana Mimi, Bwana, napenda haki, 2 na ninachukia unyangʼanyi na uovu. 1 Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao 2 na kufanya agano la milele nao. 1

9Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa, 2 na uzao wao miongoni mwa kabila za watu. 1 Wale wote watakaowaona watatambua 2 kuwa ni taifa ambalo Bwana amelibariki.” 1

10Ninafurahia sana katika Bwana, 2 nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu. 1 Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu, 2 na kunipamba kwa joho la haki, 1 kama vile bwana arusi apambavyo 2 kichwa chake kama kuhani, 1 na kama bibi arusi ajipambavyo 2 kwa vito vyake vya thamani. 1

11Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota, 2 na bustani isababishavyo mbegu kuota, 1 ndivyo Bwana Mwenyezi atafanya haki na sifa 2 zichipuke mbele ya mataifa yote.

← Isaiah 60Read In The App, Free →Isaiah 62 →

Study Isaiah 61

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566