Isaiah 48
1“Sikilizeni hili, ee nyumba ya Yakobo, 2 ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli, 2 na mnaotoka katika ukoo wa Yuda, 1 ninyi mnaoapa kwa jina la Bwana, 2 mnaomwomba Mungu wa Israeli, 2 lakini si katika kweli au kwa haki; 1
2ninyi mnaojiita raiya wa mji mtakatifu, 2 na kumtegemea Mungu wa Israeli, 2 Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake: 1
3Nilitoa unabii mambo ya kwanza tangu zamani, 2 kinywa changu kiliyatangaza na kuyafanya yajulikane; 2 kisha ghafula nikayatenda, nayo yakatokea. 1
4Kwa kuwa nalijua jinsi ulivyokuwa mkaidi; 2 mishipa ya shingo yako ilikuwa chuma, 2 kipaji chako cha uso kilikuwa shaba. 1
5Kwa hiyo nilikuambia mambo haya tangu zamani, 2 kabla hayajatokea nilikutangazia 1 ili usije ukasema, 2 ‘Sanamu zangu zilifanya hayo; 2 kinyago changu cha mti na mungu wangu wa chuma aliyaamuru.’ 1
6Umesikia mambo haya; yaangalie hayo yote. 2 Je, hutayakubali? 1 “Kuanzia sasa na kuendelea nitakueleza mambo mapya, 2 juu ya mambo yaliyofichika usiyoyajua. 1
7Yameumbwa sasa, wala si tangu zamani; 2 hukupata kuyasikia kabla ya siku ya leo. 1 Hivyo huwezi kusema, 2 ‘Naam, niliyajua hayo.’ 1
8Hujayasikia wala kuyaelewa, 2 tangu zamani sikio lako halikufunguka. 1 Ninafahamu vyema jinsi ulivyo mdanganyifu, 2 uliitwa mwasi tangu kuzaliwa kwako. 1
9Kwa ajili ya Jina langu mwenyewe 2 ninaichelewesha ghadhabu yangu, 1 kwa ajili ya sifa zangu nimeizuia isikupate, 2 ili nisije nikakukatilia mbali. 1
10Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha, 2 nimekujaribu katika tanuru ya mateso. 1
11Kwa ajili yangu mwenyewe, 2 kwa ajili yangu mwenyewe, nafanya hili. 1 Jinsi gani niliache Jina langu lichafuliwe? 2 Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine. 1 Israeli Anawekwa Huru 1
12“Ee Yakobo, nisikilize mimi, 2 Israeli, ambaye nimekuita: 1 Mimi ndiye; 2 mimi ndimi mwanzo na mwisho. 1
13Mkono wangu mwenyewe uliweka misingi ya dunia, 2 nao mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu; 2 niziitapo, zote husimama pamoja. 1
14“Kusanyikeni, ninyi nyote, msikilize: 2 Ni ipi miongoni mwa hizo sanamu 2 ambayo imetabiri vitu hivi? 1 Watu wa Bwana waliochaguliwa na kuungana 2 watatimiza kusudi lake dhidi ya Babeli; 2 mkono wa Mungu utakuwa dhidi ya Wakaldayo. 1
15Mimi, naam, Mimi, nimenena; 2 naam, nimemwita yeye. 1 Nitamleta, 2 naye atafanikiwa katika lile nililomtuma.
16“Nikaribieni na msikilize hili: 1 “Tangu tangazo la kwanza sikusema kwa siri; 2 wakati litokeapo, nitakuwako hapo.” 1 Sasa Bwana Mwenyezi amenituma, 2 kwa Roho wake. 1
17Hili ndilo asemalo Bwana, 2 Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: 1 “Mimi ni Bwana, Mungu wako, 2 nikufundishaye ili upate faida, 2 nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea. 1
18Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu, 2 amani yako ingekuwa kama mto, 2 haki yako kama mawimbi ya bahari. 1
19Wazao wako wangekuwa kama mchanga, 2 watoto wako kama chembe zake zisizohesabika; 1 kamwe jina lao lisingefutiliwa mbali, 2 wala kuangamizwa kutoka mbele zangu.” 1
20Tokeni huko Babeli, 2 kimbieni kutoka kwa Wakaldayo! 1 Tangazeni hili kwa kelele za shangwe 2 na kulihubiri. 1 Lipelekeni mpaka miisho ya dunia; 2 semeni, “ Bwana amemkomboa 2 mtumishi wake Yakobo.” 1
21Hawakuona kiu alipowaongoza kupita jangwani; 2 alifanya maji yatiririke kutoka kwenye mwamba kwa ajili yao; 1 akapasua mwamba 2 na maji yakatoka kwa nguvu. 1
22“Hakuna amani kwa waovu,” asema Bwana.