Isaiah 16
1Pelekeni wana-kondoo kama ushuru 2 kwa mtawala wa nchi, 1 Kutoka Sela, kupitia jangwani, 2 hadi mlima wa Binti Sayuni. 1
2Kama ndege wanaopapatika 2 waliofukuzwa kutoka kwenye kiota, 1 ndivyo walivyo wanawake wa Moabu 2 kwenye vivuko vya Arnoni. 1
3“Tupeni shauri, 2 toeni uamuzi. 1 Wakati wa adhuhuri, 2 fanyeni kivuli chenu kama usiku. 1 Waficheni watoro, 2 msisaliti wakimbizi. 1
4Waacheni watoro wa Moabu wakae pamoja nanyi; 2 kuweni mahali pao pa salama ili kuepuka mharabu.” 1 Mtesi atafikia mwisho na maangamizi yatakoma, 2 aletaye vita atatoweka kutoka nchi. 1
5Kwa upendo kiti cha enzi kitaimarishwa, 2 kwa uaminifu mtu ataketi juu yake, 2 yeye atokaye nyumba ya Daudi: 1 yeye ambaye katika kuhukumu hutafuta haki, 2 na huhimiza njia ya haki. 1
6Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: 2 kiburi chake cha kujivuna na udanganyifu, 1 kiburi chake na ufidhuli wake, 2 lakini majivuno yake si kitu. 1
7Kwa hiyo Wamoabu wanaomboleza, 2 wanaiombolezea Moabu kwa pamoja. 1 Wanaomboleza na kuhuzunika 2 kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. 1
8Mashamba ya Heshboni yananyauka, 2 pia na mizabibu ya Sibma. 1 Watawala wa mataifa 2 wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana, 1 ambayo ilipata kufika Yazeri 2 na kuenea kuelekea jangwani. 1 Machipukizi yake yalienea 2 yakafika hadi baharini. 1
9Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo, 2 kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. 1 Ee Heshboni, ee Eleale, 2 ninakulowesha kwa machozi! 1 Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva 2 na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa. 1
10Furaha na shangwe zimeondolewa 2 kutoka mashamba ya matunda; 1 hakuna yeyote aimbaye wala apazaye sauti 2 katika mashamba ya mizabibu; 1 hakuna yeyote akanyagaye zabibu shinikizoni, 2 kwa kuwa nimekomesha makelele. 1
11Moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama kinubi, 2 nafsi yangu yote kwa ajili ya Kir-Haresethi. 1
12Wakati Moabu anapojitokeza mahali pake pa juu, 2 anajichosha mwenyewe tu; 1 anapokwenda mahali pake pa kuabudia miungu ili kuomba, 2 haitamfaidi lolote.
13Hili ndilo neno ambalo Bwana ameshasema kuhusu Moabu.
14Lakini sasa Bwana anasema: “Katika miaka mitatu, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, fahari ya Moabu na watu wake wengi watadharauliwa, nao walionusurika watakuwa wachache sana, tena wanyonge.”