Isaiah 24
1Tazama, Bwana ataifanya dunia kuwa ukiwa 2 na kuiharibu, 1 naye atauharibu uso wake 2 na kutawanya wakaao ndani yake: 1
2ndivyo itakavyokuwa 2 kwa makuhani na kwa watu, 2 kwa bwana na kwa mtumishi, 2 kwa bibi na kwa mtumishi wake wa kike, 2 kwa muuzaji na kwa mnunuzi, 2 kwa mkopaji na kwa mkopeshaji, 2 kwa mdaiwa na kwa mdai. 1
3Dunia itaharibiwa kabisa 2 na kutekwa nyara kabisa. 4 Bwana amesema neno hili. 1
4Dunia inakauka na kunyauka, 2 dunia inanyongʼonyea na kunyauka, 2 waliotukuzwa wa dunia wananyongʼonyea. 1
5Dunia imetiwa unajisi na watu wake; 2 wameacha kutii sheria, 1 wamevunja amri 2 na kuvunja agano la milele. 1
6Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia, 2 watu wake lazima waichukue hatia yao. 1 Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa, 2 nao waliosalia ni wachache sana. 1
7Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka, 2 watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni. 1
8Furaha ya matoazi imekoma, 2 kelele za wenye furaha zimekoma, 2 shangwe za kinubi zimenyamaza. 1
9Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo, 2 kileo ni kichungu kwa wanywaji wake. 1
10Mji ulioharibiwa umekuwa ukiwa, 2 mlango wa kila nyumba umefungwa. 1
11Barabarani wanalilia kupata mvinyo, 2 furaha yote imegeuka kuwa majonzi, 2 furaha yote imefukuziwa mbali na dunia. 1
12Mji umeachwa katika uharibifu, 2 lango lake limevunjwa vipande. 1
13Ndivyo itakavyokuwa duniani 2 na miongoni mwa mataifa, 1 kama vile wakati mzeituni upigwavyo, 2 au kama vile wakati masazo yabakiavyo baada ya zabibu kuvunwa. 1
14Wanainua sauti zao, wanapiga kelele kwa furaha, 2 kutoka magharibi wanasifu kwa ukelele utukufu wa Bwana. 1
15Kwa hiyo upande wa mashariki mpeni Bwana utukufu, 2 liadhimisheni jina la Bwana, Mungu wa Israeli, 2 katika visiwa vya bahari. 1
16Kutoka miisho ya dunia tunasikia uimbaji: 2 “Utukufu kwa Yule Mwenye Haki.” 1 Lakini nilisema, “Ninadhoofika, ninadhoofika! 2 Ole wangu! 1 Watenda hila wanasaliti! 2 Kwa hila watenda hila wanasaliti!” 1
17Hofu, shimo na mtego vinakungojea, 2 ewe mtu ukaaye duniani. 1
18Kila akimbiaye asikiapo sauti ya hofu 2 atatumbukia shimoni, 1 naye yeyote apandaye kutoka shimoni, 2 atanaswa kwenye mtego. 1 Malango ya gharika ya mbinguni yamefunguliwa, 2 misingi ya dunia inatikisika. 1
19Dunia imepasuka, 2 dunia imechanika, 2 dunia imetikiswa kabisa. 1
20Dunia inapepesuka kama mlevi, 2 inayumbayumba kama kibanda kwenye upepo; 1 imelemewa sana na mzigo wa hatia ya uasi wake 2 na ikianguka kamwe haitainuka tena. 1
21Katika siku ile Bwana ataadhibu 2 nguvu zilizoko mbinguni juu, 2 na wafalme walioko duniani chini. 1
22Watakusanywa pamoja 2 kama wafungwa waliofungwa gerezani, 1 watafungiwa gerezani 2 na kuadhibiwa baada ya siku nyingi. 1
23Mwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa; 2 kwa maana Bwana Mwenye Nguvu Zote atawala 1 juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu, 2 tena mbele ya wazee wake kwa utukufu.