Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 53

1Ni nani aliyeamini ujumbe wetu, 2 na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani? 1

2Alikua mbele yake kama mche mwororo 2 na kama mzizi katika nchi kavu. 1 Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake, 2 hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani. 1

3Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu, 2 mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso. 1 Kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, 2 alidharauliwa, wala hatukumhesabu kuwa kitu. 1

4Hakika alichukua udhaifu wetu 2 na akajitwika huzuni zetu, 1 hata hivyo tulidhania kuwa amepigwa na Mungu, 2 akapigwa sana naye, na kuteswa. 1

5Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, 2 alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu; 1 adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, 2 na kwa majeraha yake sisi tumepona. 1

6Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, 2 kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, 1 naye Bwana aliweka juu yake 2 maovu yetu sisi sote. 1

7Alionewa na kuteswa, 2 hata hivyo hakufungua kinywa chake; 1 aliongozwa kama mwana-kondoo 2 apelekwaye machinjoni, 1 kama vile kondoo anyamazavyo mbele ya wao wamkataye manyoya, 2 hivyo hakufungua kinywa chake. 1

8Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa. 2 Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? 1 Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai, 2 alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu. 1

9Wakamfanyia kaburi pamoja na waovu, 2 pamoja na matajiri katika kifo chake, 1 ingawa hakutenda jeuri, 2 wala hapakuwa na hila kinywani mwake. 1

10Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana 2 kumchubua na kumsababisha ateseke. 1 Ingawa Bwana amefanya maisha yake 2 kuwa sadaka ya hatia, 1 ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, 2 nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake. 1

11Baada ya maumivu ya nafsi yake, 2 ataona nuru ya uzima na kuridhika; 1 kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye haki 2 atawafanya wengi kuwa wenye haki, 2 naye atayachukua maovu yao. 1

12Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu, 2 naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu, 1 kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti, 2 naye alihesabiwa pamoja na wakosaji. 1 Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi, 2 na kuwaombea wakosaji.

← Isaiah 52Read In The App, Free →Isaiah 54 →

Study Isaiah 53

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566