Isaiah 54
1“Imba, ewe mwanamke tasa, 2 wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; 1 paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, 2 wewe ambaye kamwe hukupata utungu; 1 kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi 2 kuliko wa mwanamke mwenye mume,” 4 asema Bwana. 1
2“Panua mahali pa hema lako, 2 tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali, 2 wala usiyazuie; 1 ongeza urefu wa kamba zako, 2 imarisha vigingi vyako. 1
3Kwa maana utaenea upande wa kuume 2 na upande wa kushoto; 1 wazao wako watayamiliki mataifa 2 na kukaa katika miji yao iliyoachwa ukiwa. 1
4“Usiogope, wewe hutaaibika. 2 Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa. 1 Wewe utasahau aibu ya ujana wako, 2 wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako. 1
5Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako, 2 Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake, 1 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako, 2 yeye anaitwa Mungu wa dunia yote. 1
6Bwana atakuita urudi 2 kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; 1 kama mke aliyeolewa bado angali kijana 2 na kukataliwa,” asema Mungu wako. 1
7“Kwa kitambo kidogo nilikuacha, 2 lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha. 1
8Katika ukali wa hasira 2 nilikuficha uso wangu kwa kitambo, 1 lakini kwa fadhili za milele 2 nitakuwa na huruma juu yako,” 2 asema Bwana Mkombozi wako. 1
9“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa, 2 nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia. 1 Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi, 2 kamwe sitawakemea tena. 1
10Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe, 2 hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika, 1 wala agano langu la amani halitaondolewa,” 2 asema Bwana, mwenye huruma juu yenu. 1
11“Ewe mji uliyeteswa, uliyepigwa kwa dhoruba na usiyetulizwa, 2 nitakujenga kwa almasi, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi. 1
12Nitafanya minara yako ya akiki, 2 malango yako kwa vito vingʼaavyo, 2 nazo kuta zako zote za vito vya thamani. 1
13Watoto wako wote watafundishwa na Bwana, 2 nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu. 1
14Kwa haki utathibitika: 1 Kuonewa kutakuwa mbali nawe; 2 hutaogopa chochote. 1 Hofu itakuwa mbali nawe; 2 haitakukaribia wewe. 1
15Kama mtu yeyote akikushambulia, 2 haitakuwa kwa ruhusa yangu; 1 yeyote akushambuliaye 2 atajisalimisha kwako. 1
16“Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi, 2 yeye afukutaye makaa kuwa moto, 2 na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake. 1 Tena ni mimi niliyemwambia mharabu 2 kufanya uharibifu mwingi. 1
17Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako 2 itakayofanikiwa, 1 nawe utauthibitisha kuwa mwongo 2 kila ulimi utakaokushtaki. 1 Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana 2 na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,” 4 asema Bwana.