Isaiah 46
1Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama; 2 sanamu zao zabebwa na wanyama wa mizigo. 1 Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea, 2 mzigo kwa waliochoka. 1
2Vinyago pamoja na wale wanaovibeba wanainama chini; 2 hiyo miungu haiwezi kuwaokoa watu, 2 wote wanakwenda utumwani pamoja. 1
3“Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo, 2 ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli, 1 ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba, 2 nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu. 1
4Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye, 2 Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi. 1 Nimewahuluku, nami nitawabeba, 2 nitawasaidia ninyi na kuwaokoa. 1
5“Mtanilinganisha na nani, au mtanihesabu kuwa sawa na nani? 2 Ni nani mtakayenifananisha naye ili tuweze kulinganishwa? 1
6Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao, 2 na kupima fedha kwenye mizani; 1 huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu, 2 kisha huisujudia na kuiabudu. 1
7Huiinua mabegani na kuichukua; 2 huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo. 2 Wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale. 1 Ingawa mtu huililia, haimjibu; 2 haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake. 1
8“Kumbukeni hili, litieni akilini, 2 liwekeni moyoni, enyi waasi. 1
9Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale; 2 mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine; 1 mimi ndimi Mungu, 2 wala hakuna mwingine aliye kama mimi. 1
10Ni mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo, 2 naam, tangu zamani za kale, 2 mambo ambayo hayajatendeka. 1 Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, 2 nami nitatenda mapenzi yangu yote. 1
11Kutoka mashariki ninaita ndege awindaye; 2 kutoka nchi ya mbali, 2 mtu atakayetimiza kusudi langu. 1 Lile ambalo nimelisema, ndilo nitakalolitimiza; 2 lile nililolipanga, ndilo nitakalolitenda. 1
12Nisikilizeni, ninyi wenye mioyo migumu, 2 ninyi mlio mbali na haki. 1
13Ninaleta haki yangu karibu, 2 haiko mbali; 2 wala wokovu wangu hautachelewa. 1 Nitawapa Sayuni wokovu, 2 Israeli utukufu wangu.