Isaiah 1
1Maono kuhusu Yuda na Yerusalemu ambayo Isaya mwana wa Amozi aliyaona wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda. 1 Taifa Asi 1
2Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia! 2 Kwa maana Bwana amesema: 1 “Nimewalisha watoto na kuwalea, 2 lakini wameniasi mimi. 1
3Ngʼombe anamjua bwana wake, 2 naye punda anajua hori la mmiliki wake, 1 lakini Israeli hajui, 2 watu wangu hawaelewi.” 1
4Lo! Taifa lenye dhambi, 2 watu waliolemewa na uovu, 1 uzao wa watenda mabaya, 2 watoto waliozoelea upotovu! 1 Wamemwacha Bwana, 2 Wamemkataa kwa dharau 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli 2 na kumgeuzia kisogo. 1
5Kwa nini mzidi kupigwa? 2 Kwa nini kudumu katika uasi? 1 Kichwa chako chote kimejeruhiwa, 2 moyo wako wote ni mgonjwa. 1
6Kutoka wayo wako wa mguu hadi kwenye utosi wa kichwa chako 2 hakuna uzima: 1 ni majeraha matupu na makovu 2 na vidonda vitokavyo damu, 1 havikusafishwa au kufungwa 2 wala kulainishwa kwa mafuta. 1
7Nchi yenu imekuwa ukiwa, 2 miji yenu imeteketezwa kwa moto; 1 nchi yenu imeachwa tupu na wageni 2 mbele ya macho yenu, 2 imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni. 1
8Binti Sayuni ameachwa kama kipenu 2 katika shamba la mizabibu, 1 kama kibanda katika shamba la matikitimaji, 2 kama mji uliohusuriwa. 1
9Kama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote + 1:9 Bwana Mwenye Nguvu Zote hapa ni Yehova Sabaoth, yaani Bwana wa Majeshi; pia Warumi 9:29 na Yakobo 5:4. 2 asingelituachia walionusurika, 1 tungelikuwa kama Sodoma, 2 tungelifanana na Gomora. 1
10Sikieni neno la Bwana, 2 ninyi watawala wa Sodoma; 1 sikilizeni sheria ya Mungu wetu, 2 enyi watu wa Gomora! 1
11Bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu, 2 ni kitu gani kwangu? 1 Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi, 2 za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona. 1 Sipendezwi na damu za mafahali 2 wala za wana-kondoo na mbuzi. 1
12Mnapokuja kujihudhurisha mbele zangu, 2 ni nani aliyewataka ninyi mfanye hivyo, 2 huku kuzikanyaga nyua zangu? 1
13Acheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana! 2 Uvumba wenu ni chukizo kwangu. 1 Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada: 2 siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu. 1
14Sikukuu zenu za Miandamo ya Mwezi, na sikukuu zenu zilizoamriwa: 2 moyo wangu unazichukia. 1 Zimekuwa mzigo kwangu, 2 nimechoka kuzivumilia. 1
15Mnaponyoosha mikono yenu katika maombi, 2 nitaficha macho yangu nisiwaone; 1 hata mkiomba maombi mengi 2 sitasikiliza. 1 Mikono yenu imejaa damu; 2
16jiosheni na mkajitakase. 1 Yaondoeni matendo yenu maovu 2 mbele zangu! 1 Acheni kutenda mabaya, 2
17jifunzeni kutenda mema! 1 Tafuteni haki, 2 watieni moyo walioonewa. 1 Teteeni shauri la yatima, 2 wateteeni wajane. 1
18“Njooni basi tuhojiane,” 2 asema Bwana. 1 “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, 2 zitakuwa nyeupe kama theluji; 1 ingawa ni nyekundu sana kama damu, 2 zitakuwa nyeupe kama sufu. 1
19Kama mkikubali na kutii, 2 mtakula mema ya nchi, 1
20lakini kama mkikataa na kuasi, 2 mtaangamizwa kwa upanga.” 4 Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena. 1
21Tazama jinsi mji uliokuwa mwaminifu 2 umekuwa kahaba! 1 Mwanzoni ulikuwa umejaa unyofu, 2 haki ilikuwa inakaa ndani yake, 2 lakini sasa ni wauaji! 1
22Fedha yenu imekuwa takataka, 2 divai yenu nzuri imechanganywa na maji. 1
23Watawala wenu ni waasi, 2 rafiki wa wevi, 1 wote wanapenda rushwa 2 na kukimbilia hongo. 1 Hawatetei yatima, 2 shauri la mjane haliletwi mbele yao lisikilizwe. 1
24Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 Mwenye Nguvu wa Israeli, asema hivi: 1 “Lo, nitapata faraja kutoka kwa adui zangu 2 na kujilipizia kisasi juu ya watesi wangu. 1
25Nitauelekeza mkono wangu dhidi yenu, 2 nitawasafisha takataka zenu zote 2 na kuwaondolea unajisi wenu wote. 1
26Nitawarudishia waamuzi wenu kama ilivyokuwa siku za zamani, 2 nao washauri wenu kama ilivyokuwa mwanzoni. 1 Baadaye utaitwa, 2 Mji wa Haki, 2 Mji Mwaminifu.” 1
27Sayuni itakombolewa kwa haki, 2 wale waliomo ndani yake waliotubu kwa uaminifu. 1
28Lakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa, 2 nao wanaomwacha Bwana wataangamia. 1
29“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni 2 ambayo mlifurahia, 1 mtafadhaika kwa sababu ya bustani 2 mlizozichagua. 1
30Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka, 2 kama bustani isiyokuwa na maji. 1
31Mtu mwenye nguvu atatoweka kama majani makavu yawakayo moto, 2 na kazi yake kama cheche ya moto; 1 vyote vitaungua pamoja, 2 wala hakuna wa kuuzima huo moto.”