Isaiah 63
1Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, 2 kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu? 1 Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari, 2 anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake? 1 “Mimi ndimi, nisemaye katika haki, 2 mwenye nguvu wa kuokoa.” 1
2Kwa nini mavazi yako ni mekundu, 2 kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu? 1
3“Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu; 2 kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami. 1 Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu 2 na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu; 1 damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu, 2 na kutia madoa nguo zangu zote. 1
4Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu, 2 mwaka wa ukombozi wangu umefika. 1
5Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia, 2 nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada; 1 hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu, 2 na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza. 1
6Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu, 2 katika ghadhabu yangu niliwalewesha, 2 na kumwaga damu yao juu ya ardhi.” 1 Kusifu Na Kuomba 1
7Nitasimulia juu ya wema wa Bwana, 2 kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, 1 sawasawa na yote ambayo Bwana 2 ametenda kwa ajili yetu: 1 naam, mambo mengi mema aliyoyatenda 2 kwa ajili ya nyumba ya Israeli, 1 sawasawa na huruma zake 2 na wema wake mwingi. 1
8Alisema, “Hakika wao ni watu wangu, 2 wana ambao hawatanidanganya”; 2 hivyo akawa Mwokozi wao. 1
9Katika taabu zao zote naye alitaabika, 2 na malaika wa uso wake akawaokoa. 1 Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa, 2 akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita. 1
10Lakini waliasi, 2 na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake. 1 Hivyo aligeuka na kuwa adui yao, 2 na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao. 1
11Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita, 2 siku za Mose na watu wake: 1 yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari, 2 pamoja na wachungaji wa kundi lake? 1 Yuko wapi yule aliyeweka 2 Roho wake Mtakatifu katikati yao, 1
12aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu 2 kuwa katika mkono wa kuume wa Mose, 1 aliyegawa maji ya bahari mbele yao, 2 ili kujipatia jina milele, 1
13aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi? 2 Kama farasi katika nchi iliyo wazi, 2 wao hawakujikwaa, 1
14kama ngʼombe washukao bondeni kwenye malisho, 2 walipewa pumziko na Roho wa Bwana. 1 Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako 2 ili kujipatia mwenyewe jina tukufu. 1
15Tazama chini kutoka mbinguni ukaone 2 kutoka kiti chako cha enzi 2 kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu. 1 Uko wapi wivu wako na uweza wako? 2 Umetuzuilia wema wako na huruma zako. 1
16Lakini wewe ni Baba yetu, 2 ingawa Abrahamu hatufahamu sisi 2 wala Israeli hatutambui; 1 wewe, Ee Bwana, ndiwe Baba yetu, 2 Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako. 1
17Ee Bwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako, 2 na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu? 1 Rudi kwa ajili ya watumishi wako, 2 yale makabila ambayo ni urithi wako. 1
18Kwa maana kwa muda mfupi watu wako walimiliki mahali pako patakatifu, 2 lakini sasa adui zetu wamepakanyaga mahali patakatifu pako. 1
19Sisi tumekuwa kama wale ambao hujawatawala kamwe, 1 kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.