Isaiah 35
1Jangwa na nchi kame vitafurahi; 2 nyika itashangilia na kuchanua maua. 1 Kama waridi,
2litachanua maua, 2 litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha. 1 Litapewa utukufu wa Lebanoni, 2 fahari ya Karmeli na Sharoni; 1 wataona utukufu wa Bwana, 2 fahari ya Mungu wetu. 1
3Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, 2 yafanyeni imara magoti yaliyolegea, 1
4waambieni wale wenye mioyo ya hofu, 2 “Kuweni hodari, msiogope; 1 tazama, Mungu wenu atakuja, 2 pamoja na malipo ya Mungu, 2 atakuja na kuwaokoa ninyi.” 1
5Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa 2 na masikio ya viziwi yatazibuliwa. 1
6Ndipo kilema atarukaruka kama kulungu, 2 nao ulimi wa aliye bubu utapaza sauti kwa shangwe. 1 Maji yatatiririka kwa kasi katika nyika, 2 na vijito katika jangwa. 1
7Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji, 2 ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi. 1 Maskani ya mbweha walikolala hapo awali 2 patamea majani, matete na mafunjo. 1
8Nako kutakuwa na njia kuu, 2 nayo itaitwa Njia ya Utakatifu. 1 Wasio safi hawatapita juu yake; 2 itakuwa ya wale watembeao katika Njia ile; 1 yeye asafiriye juu yake, 2 ajapokuwa mjinga, hatapotea. 1
9Huko hakutakuwepo na simba, 2 wala mnyama mkali hatapita njia hiyo, 2 wala hawatapatikana humo. 1 Ila waliokombolewa tu ndio watakaopita huko, 2
10waliokombolewa na Bwana watarudi. 1 Wataingia Sayuni wakiimba; 2 furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao. 1 Watapata furaha na shangwe; 2 huzuni na majonzi vitakimbia.