Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 45

1“Hili ndilo asemalo Bwana kwa mpakwa mafuta wake, 2 Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume 1 kutiisha mataifa mbele yake 2 na kuwavua wafalme silaha zao, 1 kufungua milango mbele yake 2 ili malango yasije yakafungwa: 1

2Nitakwenda mbele yako 2 na kusawazisha milima; 1 nitavunjavunja malango ya shaba 2 na kukatakata mapingo ya chuma. 1

3Nitakupa hazina za gizani, 2 mali zilizofichwa mahali pa siri, 1 ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimi Bwana, 2 Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako. 1

4Kwa ajili ya Yakobo mtumishi wangu, 2 Israeli niliyemchagua, 1 nimekuita wewe kwa jina lako, 2 na kukupa jina la heshima, 2 ingawa wewe hunitambui. 1

5Mimi ndimi Bwana, wala hakuna mwingine, 2 zaidi yangu hakuna Mungu. 1 Nitakutia nguvu, 2 ingawa wewe hujanitambua, 1

6ili kutoka mawio ya jua 2 mpaka machweo yake, 1 watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi. 2 Mimi ndimi Bwana wala hakuna mwingine. 1

7Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, 2 ninaleta mafanikio na kusababisha maafa. 2 Mimi, Bwana, huyatenda haya yote. 1

8“Enyi mbingu juu, nyesheni haki, 2 mawingu na yaidondoshe. 1 Dunia na ifunguke sana, 2 wokovu na uchipuke, 1 haki na ikue pamoja nao. 2 Mimi, Bwana, ndiye niliyeiumba. 1

9“Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake, 2 yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi. 1 Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi, 2 ‘Unatengeneza nini wewe?’ 2 Je, kazi yako husema, 1 ‘Hana mikono’? 1

10Ole wake amwambiaye baba yake, 2 ‘Umezaa nini?’ 2 Au kumwambia mama yake, 2 ‘Umezaa kitu gani?’ 1

11“Hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na Muumba wake: 1 Kuhusu mambo yatakayokuja, 2 je, unaniuliza habari za watoto wangu, 2 au kunipa amri kuhusu kazi za mikono yangu? 1

12Mimi ndiye niliyeumba dunia 2 na kumuumba mwanadamu juu yake. 1 Mikono yangu mwenyewe ndiyo iliyozitanda mbingu, 2 nikayapanga majeshi yake yote ya angani. 1

13Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu: 2 nitazinyoosha njia zake zote. 1 Yeye atajenga mji wangu upya, 2 na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni, 1 lakini si kwa kulipiwa fedha wala kupewa zawadi, 2 asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

14Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi, 2 nao wale Waseba warefu, 1 watakujia na kuwa wako, 2 watakujia wakijikokota nyuma yako, 2 watakujia wamefungwa minyororo. 1 Watasujudu mbele yako 2 wakikusihi na kusema, 1 ‘Hakika Mungu yu pamoja nawe, 2 wala hakuna mwingine; 2 hakuna Mungu mwingine.’ ” 1

15Hakika wewe u Mungu unayejificha, 2 Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli. 1

16Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika; 2 wataenda kutahayarika pamoja. 1

17Lakini Israeli ataokolewa na Bwana 2 kwa wokovu wa milele; 1 kamwe hutaaibika wala kutatahayarika, 2 milele yote. 1

18Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye aliyeumba mbingu, 2 ndiye Mungu; 1 yeye aliyeifanya dunia na kuiumba, 2 yeye ndiye aliiwekea misingi imara, 1 hakuiumba ili iwe tupu, 2 bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake. 1 Anasema: 2 “Mimi ndimi Bwana, 2 wala hakuna mwingine. 1

19Sijasema sirini, 2 kutoka mahali fulani katika nchi ya giza; 1 sijawaambia wazao wa Yakobo, 2 ‘Nitafuteni bure.’ 1 Mimi, Bwana, nasema kweli; 2 ninatangaza lililo sahihi. 1

20“Kusanyikeni pamoja mje, 2 enyi wakimbizi kutoka mataifa. 1 Wale wabebao sanamu za mti ni watu wasio na akili, 2 wale waombao miungu isiyoweza kuokoa. 1

21Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo, 2 wao na wafanye shauri pamoja. 1 Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, 2 aliyetangaza tangu zamani za kale? 1 Je, haikuwa Mimi, Bwana? 2 Wala hapana Mungu mwingine 2 zaidi yangu mimi, 1 Mungu mwenye haki na Mwokozi; 2 hapana mwingine ila mimi. 1

22“Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe, 2 enyi miisho yote ya dunia; 1 kwa maana mimi ndimi Mungu, 2 wala hapana mwingine. 1

23Nimeapa kwa nafsi yangu, 2 kinywa changu kimenena katika uadilifu wote 2 neno ambalo halitatanguka: 1 Kila goti litapigwa mbele zangu, 2 kwangu mimi kila ulimi utaapa. 1

24Watasema kuhusu mimi, 2 ‘Katika Bwana peke yake 2 ndiko kuna haki na nguvu.’ ” 1 Wote ambao wamemkasirikia Mungu 2 watamjia yeye, nao watatahayarika. 1

25Lakini katika Bwana wazao wote wa Israeli 2 wataonekana wenye haki na watashangilia.

← Isaiah 44Read In The App, Free →Isaiah 46 →

Study Isaiah 45

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566