Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 55

1“Njooni, ninyi nyote wenye kiu, 2 njooni kwenye maji; 1 nanyi ambao hamna fedha, 2 njooni, nunueni na mle! 1 Njooni, nunueni divai na maziwa 2 bila fedha na bila gharama. 1

2Kwa nini kutumia fedha kwa kitu ambacho si chakula, 2 na kutaabikia kitu kisichoshibisha? 1 Sikilizeni, nisikilizeni mimi na mle kilicho kizuri, 2 nazo nafsi zenu zitafurahia utajiri wa unono. 1

3Tegeni sikio mje kwangu, 2 nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi. 1 Nitafanya agano la milele nanyi, 2 pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi. 1

4Tazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa, 2 kiongozi na jemadari wa mataifa. 1

5Hakika utaita mataifa usiyoyajua, 2 nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia, 1 kwa sababu ya Bwana Mungu wako, 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, 2 kwa maana amekutukuza.” 1

6Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana; 2 mwiteni maadamu yu karibu. 1

7Mtu mwovu na aiache njia yake, 2 na mtu mbaya na ayaache mawazo yake. 1 Yeye na amrudie Bwana, naye atamrehemu, 2 arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa. 1

8“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, 2 wala njia zenu si njia zangu,” 4 asema Bwana. 1

9“Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, 2 ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu 2 na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 1

10Kama vile mvua na theluji 2 ishukavyo kutoka mbinguni, 1 nayo hairudi tena huko 2 bila kunywesha dunia 1 na kuichipusha na kuistawisha, 2 hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi 2 na mkate kwa mlaji, 1

11ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu: 2 Halitanirudia tupu, 1 bali litatimiliza lile nililokusudia 2 na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma. 1

12Mtatoka nje kwa furaha 2 na kuongozwa kwa amani; 1 milima na vilima 2 vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu, 1 nayo miti yote ya shambani 2 itapiga makofi. 1

13Badala ya kichaka cha miiba 2 itaota miti ya misunobari, 1 na badala ya michongoma 2 utaota mhadasi. + 55:13 Mhadasi ni aina ya mti ambao huota milimani karibu na Yerusalemu, hutoa harufu nzuri itumikayo kutengeneza manukato; kwa Kiebrania ni “hadas”, na ilikuwa inatumika kujenga vibanda wakati wa Sikukuu ya Vibanda (ona pia Neh 8:15 ). 1 Hili litakuwa jambo la kumpatia Bwana jina, 2 kwa ajili ya ishara ya milele, 2 ambayo haitaharibiwa.”

← Isaiah 54Read In The App, Free →Isaiah 56 →

Study Isaiah 55

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566