Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 25

1Ee Bwana, wewe ni Mungu wangu, 2 nitakutukuza na kulisifu jina lako, 1 kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu 2 umetenda mambo ya ajabu, 2 mambo yaliyokusudiwa tangu zamani. 1

2Umeufanya mji kuwa lundo la kifusi, 2 mji wenye ngome kuwa magofu, 1 ngome imara ya wageni kuwa si mji tena, 2 wala hautajengwa tena kamwe. 1

3Kwa hiyo mataifa yenye nguvu yatakuheshimu, 2 miji ya mataifa katili itakuheshimu wewe. 1

4Umekuwa kimbilio la watu maskini, 2 kimbilio la mhitaji katika taabu yake, 1 hifadhi wakati wa dhoruba 2 na kivuli wakati wa hari. 1 Kwa maana pumzi ya wakatili 2 ni kama dhoruba ipigayo ukuta 2

5na kama joto la jangwani. 1 Wewe wanyamazisha makelele ya wageni; 2 kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu, 2 ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo. 1

6Juu ya mlima huu Bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa 2 karamu ya vinono kwa mataifa yote, 1 karamu ya mvinyo wa zamani, 2 nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana. 1

7Juu ya mlima huu ataharibu 2 sitara ihifadhiyo mataifa yote, 1 kile kifuniko kifunikacho mataifa yote, 2

8yeye atameza mauti milele. 1 Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote; 2 ataondoa aibu ya watu wake duniani kote. 4 Bwana amesema hili. 1

9Katika siku ile watasema, 2 “Hakika huyu ndiye Mungu wetu; 2 tulimtumaini, naye akatuokoa. 1 Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini; 2 sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.” 1

10Mkono wa Bwana utatulia juu ya mlima huu, 2 bali Moabu atakanyagwa chini 2 kama majani makavu yakanyagwavyo kwenye shimo la mbolea. 1

11Watakunjua mikono yao katikati yake, 2 kama vile mwogeleaji akunjuavyo mikono yake ili aogelee. 1 Mungu atashusha kiburi chao 2 licha ya ujanja wa mikono yao. 1

12Atabomoa kuta ndefu za maboma yako 2 na kuziangusha chini, 1 atazishusha chini ardhini, 2 mpaka mavumbini kabisa.

← Isaiah 24Read In The App, Free →Isaiah 26 →

Study Isaiah 25

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566