Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 42

1“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, 2 mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye; 1 nitaweka Roho yangu juu yake, 2 naye ataleta haki kwa mataifa. 1

2Hatapaza sauti wala kupiga kelele, 2 wala hataiinua sauti yake barabarani. 1

3Mwanzi uliopondeka hatauvunja, 2 na utambi unaofuka moshi hatauzima. 1 Kwa uaminifu ataleta haki, 2

4hatazimia roho wala kukata tamaa, 1 mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia. 2 Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.” 1

5Hili ndilo asemalo Mungu, Bwana, 2 yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda, 1 aliyeitandaza dunia na vyote vitokavyo humo, 2 awapaye watu wake pumzi, 2 na uzima kwa wale waendao humo: 1

6“Mimi, Bwana, nimekuita katika haki; 2 nitakushika mkono wako. 1 Nitakulinda na kukufanya 2 kuwa Agano kwa ajili ya watu 2 na nuru kwa Mataifa, 1

7kuwafungua macho wale wasioona, 2 kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela, 1 na kuwafungua kutoka gerezani 2 wale wanaokaa gizani. 1

8“Mimi ndimi Bwana; hilo ndilo Jina langu! 2 Sitampa mwingine utukufu wangu 2 wala sanamu sifa zangu. 1

9Tazama, mambo ya kwanza yametokea, 2 nami natangaza mambo mapya; 1 kabla hayajatokea 2 nawatangazia habari zake.” 1 Wimbo Wa Kumsifu Bwana 1

10Mwimbieni Bwana wimbo mpya, 2 sifa zake toka miisho ya dunia, 1 ninyi mshukao chini baharini, 2 na vyote vilivyomo ndani yake, 2 enyi visiwa na wote wakaao ndani yake. 1

11Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao; 2 makao anamoishi Kedari na yashangilie. 1 Watu wa Sela waimbe kwa furaha, 2 na wapige kelele kutoka vilele vya milima. 1

12Wampe Bwana utukufu, 2 na kutangaza sifa zake katika visiwa. 1

13Bwana ataenda kama mtu mwenye nguvu, 2 kama shujaa atachochea shauku yake, 1 kwa kelele ataamsha kilio cha vita, 2 naye atashinda adui zake. 1

14“Kwa muda mrefu nimenyamaza kimya, 2 nimekaa kimya na kujizuia. 1 Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua, 2 ninapiga kelele, ninatweta na kushusha pumzi. 1

15Nitaharibu milima na vilima 2 na kukausha mimea yako yote; 1 nitafanya mito kuwa visiwa 2 na kukausha mabwawa. 1

16Nitawaongoza vipofu kwenye njia ambayo hawajaijua, 2 kwenye mapito wasiyoyazoea nitawaongoza; 1 nitafanya giza kuwa nuru mbele yao, 2 na kufanya mahali palipoparuza kuwa laini. 1 Haya ndiyo mambo nitakayofanya; 2 mimi sitawaacha. 1

17Lakini wale wanaotumaini sanamu, 2 wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’ 2 watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa. 1 Israeli Kipofu Na Kiziwi 1

18“Sikieni, enyi viziwi; 2 tazameni, enyi vipofu, mpate kuona! 1

19Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu, 2 na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? 1 Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu, 2 aliye kipofu kama mtumishi wa Bwana? 1

20Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia; 2 masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii chochote.” 1

21Ilimpendeza Bwana 2 kwa ajili ya haki yake 2 kufanya sheria yake kuwa kuu na tukufu. 1

22Lakini hili ni taifa lililoibwa na kutekwa nyara, 2 wote wamenaswa katika mashimo, 2 au wamefichwa katika magereza. 1 Wamekuwa nyara, 2 wala hapana yeyote awaokoaye. 1 Wamefanywa mateka, 2 wala hapana yeyote asemaye, “Warudishe.” 1

23Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili, 2 au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao? 1

24Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, 2 na Israeli kwa wateka nyara? 1 Je, hakuwa yeye, Bwana, 2 ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? 1 Kwa kuwa hawakufuata njia zake, 2 hawakutii sheria zake. 1

25Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka, 2 ukali wa vita. 1 Iliwazunguka kwa miali ya moto, lakini hata hivyo hawakuelewa; 2 iliwateketeza, lakini hawakuyatia moyoni.

← Isaiah 41Read In The App, Free →Isaiah 43 →

Study Isaiah 42

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566