Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 65

1“Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia. 2 Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta. 1 Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu, 2 nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’ 1

2Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu 2 kwa watu wakaidi, 1 wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri, 2 wafuatao mawazo yao wenyewe: 1

3taifa ambalo daima hunikasirisha 2 machoni pangu, 1 wakitoa dhabihu katika bustani 2 na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali; 1

4watu waketio katikati ya makaburi 2 na kukesha mahali pa siri, 1 walao nyama za nguruwe, 2 nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi, 1

5wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie, 2 kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’ 1 Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu, 2 ni moto uwakao mchana kutwa. 1

6“Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu: 2 sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu; 2 nitalipiza mapajani mwao: 1

7dhambi zenu na dhambi za baba zenu,” 2 asema Bwana. 1 “Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima 2 na kunichokoza mimi juu ya vilima, 1 nitawapimia mapajani mwao 2 malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”

8Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana 2 katika kishada cha zabibu, 1 nao watu husema, ‘Usikiharibu, 2 kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’ 1 hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; 2 sitawaangamiza wote. 1

9Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo, 2 na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu, 1 nao watu wangu wateule watairithi, 2 nako huko wataishi watumishi wangu. 1

10Sharoni itakuwa malisho 2 kwa ajili ya makundi ya kondoo, 1 na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia 2 kwa makundi ya ngʼombe, 2 kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta. 1

11“Bali kwenu ninyi mnaomwacha Bwana 2 na kuusahau mlima wangu mtakatifu, 1 ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati, + 65:11 Bahati alikuwa mungu wa Wakaldayo ambaye pia alijulikana kama Gadi. 2 na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa 2 kwa ajili ya Ajali, + 65:11 Ajali au Meni alikuwa mungu wa majaliwa. 1

12nitawaagiza mfe kwa upanga, 2 nanyi nyote mtainama chini ili kuchinjwa; 1 kwa kuwa niliwaita lakini hamkuitika, 2 nilisema lakini hamkusikiliza. 1 Mlitenda maovu machoni pangu, 2 nanyi mkachagua mambo yale yanayonichukiza.”

13Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: 1 “Watumishi wangu watakula, 2 lakini ninyi mtaona njaa; 1 watumishi wangu watakunywa 2 lakini ninyi mtaona kiu; 1 watumishi wangu watafurahi, 2 lakini ninyi mtaona haya. 1

14Watumishi wangu wataimba 2 kwa furaha ya mioyo yao, 1 lakini ninyi mtalia 2 kutokana na uchungu wa moyoni, 1 na kupiga yowe kwa sababu 2 ya uchungu wa roho zenu. 1

15Mtaliacha jina lenu 2 kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa; 1 Bwana Mwenyezi atawaua ninyi, 2 lakini watumishi wake atawapa jina jingine. 1

16Yeye aombaye baraka katika nchi 2 atafanya hivyo kwa Mungu wa kweli; 1 yeye aapaye katika nchi 2 ataapa kwa Mungu wa kweli. 1 Kwa kuwa taabu za zamani zitasahaulika 2 na kufichwa kutoka machoni pangu. 1 Mbingu Mpya Na Dunia Mpya 1

17“Tazama, nitaumba 2 mbingu mpya na dunia mpya. 1 Mambo ya zamani hayatakumbukwa, 2 wala hayatakuja akilini. 1

18Lakini furahini na kushangilia daima 2 katika hivi nitakavyoumba, 1 kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza, 2 nao watu wake wawe furaha. 1

19Nami nitaifurahia Yerusalemu 2 na kuwafurahia watu wangu; 1 sauti ya maombolezo na ya kilio 2 haitasikika humo tena. 1

20“Kamwe hatakuwepo tena ndani yake 2 mtoto mchanga atakayeishi siku chache tu, 2 au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake. 1 Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia moja 2 atahesabiwa kwamba ni kijana tu, 1 yeye ambaye hatafika miaka mia moja, 2 atahesabiwa kuwa amelaaniwa. 1

21Watajenga nyumba na kuishi ndani yake; 2 watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake. 1

22Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake, 2 au kupanda mazao na wengine wale. 1 Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti, 2 ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, 1 wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi 2 kazi za mikono yao. 1

23Hawatajitaabisha kwa kazi bure, 2 wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, 1 kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Bwana, 2 wao na wazao wao pamoja nao. 1

24Kabla hawajaita, nitajibu, 2 nao wakiwa katika kunena, nitasikia. 1

25Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, 2 naye simba atakula nyasi kama maksai, 2 lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. 1 Hawatadhuru wala kuharibu 2 katika mlima wangu mtakatifu wote,” 4 asema Bwana.

← Isaiah 64Read In The App, Free →Isaiah 66 →

Study Isaiah 65

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566