Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 10

1Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali? 2 Kwa nini unajificha wakati wa shida? 1

2Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, 2 waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga. 1

3Hujivunia tamaa za moyo wake; 2 humbariki mlafi na kumtukana Bwana. 1

4Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, 2 katika mawazo yake yote 2 hakuna nafasi ya Mungu. 1

5Njia zake daima hufanikiwa; 2 hujivuna na amri zako ziko mbali naye, 2 huwacheka kwa dharau adui zake wote. 1

6Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa, 2 daima nitakuwa na furaha, 2 kamwe sitakuwa na shida.” 1

7Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho; 2 shida na ubaya viko chini ya ulimi wake. 1

8Huvizia karibu na vijiji; 2 kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia, 2 akivizia wapitaji. 1

9Huvizia kama simba aliye mawindoni; 2 huvizia kumkamata mnyonge, 1 huwakamata wanyonge na kuwaburuza 2 katika wavu wake. 1

10Mateka wake hupondwa, huzimia; 2 wanaanguka katika nguvu zake. 1

11Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, 2 huficha uso wake na haoni kabisa.” 1

12Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. 2 Usiwasahau wanyonge. 1

13Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? 2 Kwa nini anajiambia mwenyewe, 2 “Hataniita nitoe hesabu?” 1

14Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, 2 umekubali kuyapokea mkononi mwako. 1 Mhanga anajisalimisha kwako, 2 wewe ni msaada wa yatima. 1

15Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, 2 mwite atoe hesabu ya maovu yake 2 ambayo yasingejulikana. 1

16Bwana ni Mfalme milele na milele, 2 mataifa wataangamia watoke nchini mwake. 1

17Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa, 2 wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao, 1

18ukiwatetea yatima na walioonewa, 2 ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.

← Psalms 9Read In The App, Free →Psalms 11 →

Study Psalms 10

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150