Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 36

1Kuna neno moyoni mwangu 2 kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. 1 Hakuna hofu ya Mungu 2 mbele ya macho yake. 1

2Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno 2 hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. 1

3Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, 2 ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema. 1

4Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, 2 hujitia katika njia ya dhambi 2 na hakatai lililo baya. 1

5Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni, 2 uaminifu wako hadi kwenye anga. 1

6Haki yako ni kama milima mikubwa, 2 hukumu zako ni kama kilindi kikuu. 1 Ee Bwana, wewe huwahifadhi 2 mwanadamu na mnyama. 1

7Upendo wako usiokoma 2 ni wa thamani mno! 1 Watu wakuu na wadogo 2 hujificha uvulini wa mbawa zako. 1

8Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, 2 nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako. 1

9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, 2 katika nuru yako twaona nuru. 1

10Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, 2 haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo. 1

11Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu, 2 wala mkono wa mwovu usinifukuze. 1

12Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka: 2 wametupwa chini, hawawezi kuinuka!

← Psalms 35Read In The App, Free →Psalms 37 →

Study Psalms 36

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150