Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 49

1Sikieni haya, enyi mataifa yote, 2 sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii. 1

2Wakubwa kwa wadogo, 2 matajiri na maskini pamoja: 1

3Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, 2 usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu. 1

4Nitatega sikio langu nisikilize mithali, 2 nitafafanua kitendawili kwa zeze: 1

5Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, 2 wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka, 1

6wale wanaotegemea mali zao 2 na kujivunia utajiri wao mwingi? 1

7Hakuna mwanadamu awaye yote 2 awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, 2 au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake. 1

8Fidia ya uhai ni gharama kubwa, 2 hakuna malipo yoyote yanayotosha, 1

9ili kwamba aishi milele 2 na asione uharibifu. 1

10Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; 2 wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia 2 na kuwaachia wengine mali zao. 1

11Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, 2 makao yao vizazi vyote; 1 ingawa walikuwa na mashamba 2 na kuyaita kwa majina yao. 1

12Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; 2 anafanana na mnyama aangamiaye. 1

13Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, 2 pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao. 1

14Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, + 49:14 Kaburini hapa ina maana ya Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu. 2 nacho kifo kitawala. 1 Wanyofu watawatawala asubuhi, 2 maumbile yao yataozea kaburini, 2 mbali na majumba yao makubwa ya fahari. 1

15Lakini Mungu atakomboa uhai + 49:15 Au: nafsi. wangu na kaburi, 2 hakika atanichukua kwake. 1

16Usitishwe mtu anapotajirika, 2 fahari ya nyumba yake inapoongezeka, 1

17kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, 2 fahari yake haitashuka pamoja naye. 1

18Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, 2 na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa, 1

19atajiunga na kizazi cha baba zake, 2 ambao hawataona kamwe nuru ya uzima. 1

20Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu 2 ni kama wanyama waangamiao.

← Psalms 48Read In The App, Free →Psalms 50 →

Study Psalms 49

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150