Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 76

1Katika Yuda, Mungu anajulikana, 2 jina lake ni kuu katika Israeli. 1

2Hema lake liko Salemu, 2 makao yake katika Sayuni. 1

3Huko alivunja mishale imetametayo, 2 ngao na panga, silaha za vita. 1

4Wewe unangʼaa kwa mwanga, 2 mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori. 1

5Mashujaa hulala wametekwa nyara, 2 hulala usingizi wao wa mwisho; 1 hakuna hata mmoja wa watu wa vita 2 anayeweza kuinua mikono yake. 1

6Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, 2 farasi na gari la vita vilikaa kimya. 1

7Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa. 2 Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika? 1

8Kutoka mbinguni ulitamka hukumu, 2 nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya: 1

9wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, 2 kuwaokoa wote walioonewa katika nchi. 1

10Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa, 2 na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi. 1

11Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza; 2 nchi zote za jirani na walete zawadi 2 kwa Yule astahiliye kuogopwa. 1

12Huvunja roho za watawala; 2 anaogopwa na wafalme wa dunia.

← Psalms 75Read In The App, Free →Psalms 77 →

Study Psalms 76

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150