Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 30

1Nitakutukuza wewe, Ee Bwana, 2 kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, 1 na hukuacha adui zangu 2 washangilie juu yangu. 1

2Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie 2 na wewe umeniponya. 1

3Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, 2 umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. 1

4Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake; 2 lisifuni jina lake takatifu. 1

5Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, 2 bali upendo wake hudumu siku zote. 1 Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, 2 lakini asubuhi kukawa na furaha. 1

6Nilipofanikiwa nilisema, 2 “Sitatikiswa kamwe.” 1

7Ee Bwana, uliponijalia, 2 uliuimarisha mlima wangu, 1 lakini ulipouficha uso wako 2 nilifadhaika. 1

8Kwako wewe, Ee Bwana, niliita, 2 kwa Bwana niliomba rehema: 1

9“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? 2 Katika kushuka kwangu shimoni? 1 Je, mavumbi yatakusifu? 2 Je, yatatangaza uaminifu wako? 1

10Ee Bwana, unisikie na kunihurumia, 2 Ee Bwana, uwe msaada wangu.” 1

11Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, 2 ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe, 1

12ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. 2 Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.

← Psalms 29Read In The App, Free →Psalms 31 →

Study Psalms 30

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150