Psalms 48
1Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, 2 katika mji wa Mungu wetu, 2 mlima wake mtakatifu. 1
2Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana, 2 furaha ya dunia yote. 1 Kama vilele vya juu sana vya Safoni + 48:2 Safoni inaweza ikawa na maana ya mlima mtakatifu au upande wa kaskazini. ni Mlima Sayuni, 2 mji wa Mfalme Mkuu. 1
3Mungu yuko katika ngome zake; 2 amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake. 1
4Wakati wafalme walipounganisha nguvu, 2 waliposonga mbele pamoja, 1
5walimwona nao wakashangaa, 2 wakakimbia kwa hofu. 1
6Kutetemeka kuliwashika huko, 2 maumivu kama ya mwanamke 2 mwenye utungu wa kuzaa. 1
7Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi 2 zilizovunjwa na upepo wa mashariki. 1
8Kama tulivyokuwa tumesikia, 2 ndivyo tulivyoona 1 katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 katika mji wa Mungu wetu: 2 Mungu ataufanya uwe salama milele. 1
9Ee Mungu, hekaluni mwako 2 tunatafakari upendo wako usiokoma. 1
10Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, 2 sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, 2 mkono wako wa kuume umejazwa na haki. 1
11Mlima Sayuni unashangilia, 2 vijiji vya Yuda vinafurahi 2 kwa sababu ya hukumu zako. 1
12Tembeeni katika Sayuni, 2 uzungukeni mji, 2 hesabuni minara yake; 1
13yatafakarini vyema maboma yake, 2 angalieni ngome zake, 1 ili mpate kusimulia habari zake 2 kwa kizazi kijacho. 1
14Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; 2 atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.