Psalms 73
1Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, 2 kwa wale ambao mioyo yao ni safi. 1
2Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; 2 nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama. 1
3Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna 2 nilipoona kufanikiwa kwa waovu. 1
4Wao hawana taabu, + 73:4 Tafsiri nyingine zinasema: hawana maumivu katika kufa kwao. 2 miili yao ina afya na nguvu. 1
5Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, 2 wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine. 1
6Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, 2 wamejivika jeuri. 1
7Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi, 2 majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo. 1
8Hudhihaki na kusema kwa ukorofi, 2 katika majivuno yao wanatishia kutesa. 1
9Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu, 2 nazo ndimi zao humiliki duniani. 1
10Kwa hiyo watu wao huwageukia 2 na kunywa maji tele. + 73:10 Au: na kupokea yote wasemayo. 1
11Wanasema, “Mungu awezaje kujua? 2 Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?” 1
12Hivi ndivyo walivyo waovu: 2 siku zote hawajali, 2 wanaongezeka katika utajiri. 1
13Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, 2 ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia. 1
14Mchana kutwa nimetaabika, 2 nimeadhibiwa kila asubuhi. 1
15Kama ningesema, “Nitasema hivi,” 2 ningelikuwa nimewasaliti watoto wako. 1
16Nilipojaribu kuelewa haya yote, 2 yalikuwa magumu kwangu kuelewa. 1
17Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, 2 ndipo nilipotambua mwisho wao. 1
18Hakika unawaweka mahali pa utelezi, 2 unawaangusha chini kwa uharibifu. 1
19Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, 2 wanatoweshwa kabisa na vitisho! 1
20Kama ndoto mtu aamkapo, 2 hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, 2 utawatowesha kama ndoto. 1
21Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, 2 na roho yangu ilipotiwa uchungu, 1
22nilikuwa mpumbavu na mjinga, 2 nilikuwa mnyama mkatili mbele yako. 1
23Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, 2 umenishika mkono wangu wa kuume. 1
24Unaniongoza kwa shauri lako, 2 hatimaye utaniingiza katika utukufu. 1
25Nani niliye naye mbinguni ila wewe? 2 Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe. 1
26Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, 2 bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu 2 na fungu langu milele. 1
27Wale walio mbali nawe wataangamia, 2 unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako. 1
28Lakini kwangu mimi, 2 ni vyema kuwa karibu na Mungu. 1 Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu; 2 nami nitayasimulia matendo yako yote.