Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 90

1Bwana, wewe umekuwa makao yetu 2 katika vizazi vyote. 1

2Kabla ya kuzaliwa milima 2 au hujaumba dunia na ulimwengu, 2 wewe ni Mungu tangu milele hata milele. 1

3Huwarudisha watu mavumbini, 2 ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.” 1

4Kwa maana kwako miaka elfu 2 ni kama siku moja iliyokwisha pita, 2 au kama kesha la usiku. 1

5Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo, 2 nao ni kama majani machanga ya asubuhi: 1

6ingawa asubuhi yanachipua, 2 ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka. 1

7Tumeangamizwa kwa hasira yako 2 na tumetishwa kwa ghadhabu yako. 1

8Umeyaweka maovu yetu mbele yako, 2 dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako. 1

9Tumeishi siku zetu zote chini ya ghadhabu yako, 2 tunamaliza miaka yetu kwa kuomboleza. 1

10Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, 2 au miaka themanini ikiwa tuna nguvu, 2 lakini yote ni ya shida na taabu, 2 nazo zapita haraka, nasi twatoweka. 1

11Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako? 2 Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa 2 kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako. 1

12Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, 2 ili tujipatie moyo wa hekima. 1

13Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini? 2 Wahurumie watumishi wako. 1

14Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma, 2 ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote. 1

15Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu, 2 kulingana na miaka tuliyotaabika. 1

16Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, 2 utukufu wako kwa watoto wao. 1

17Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu; 2 uzithibitishe kazi za mikono yetu: 2 naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu.

← Psalms 89Read In The App, Free →Psalms 91 →

Study Psalms 90

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150