Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 104

1Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. 1 Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, 2 umejivika utukufu na enzi. 1

2Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, 2 amezitandaza mbingu kama hema 1

3na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. 1 Huyafanya mawingu kuwa gari lake, 2 na hupanda kwenye mbawa za upepo. 1

4Huzifanya pepo kuwa wajumbe + 104:4 Au: malaika. wake, 2 miali ya moto watumishi wake. 1

5Ameiweka dunia kwenye misingi yake, 2 haiwezi kamwe kuondoshwa. 1

6Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, 2 maji yalisimama juu ya milima. 1

7Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, 2 kwa sauti ya radi yako yakatoroka, 1

8yakapanda milima, yakateremka mabondeni, 2 hadi mahali pale ulipoyakusudia. 1

9Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, 2 kamwe hayataifunika dunia tena. 1

10Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, 2 hutiririka kati ya milima. 1

11Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, 2 punda-mwitu huzima kiu yao. 1

12Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, 2 huimba katikati ya matawi. 1

13Huinyeshea milima kutoka orofa zake, 2 dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake. 1

14Huyafanya majani ya mifugo yaote, 2 na mimea kwa watu kulima, 2 wajipatie chakula kutoka ardhini: 1

15divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, 2 mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, 2 na mkate wa kutia mwili nguvu. 1

16Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri, 2 mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. 1

17Humo ndege hufanya viota vyao, 2 korongo ana nyumba yake kwenye msunobari. 1

18Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu, 2 majabali ni kimbilio la pelele. 1

19Mwezi hugawanya majira, 2 na jua hutambua wakati wake wa kutua. 1

20Unaleta giza, kunakuwa usiku, 2 wanyama wote wa mwituni huzurura. 1

21Simba hunguruma kwa mawindo yao, 2 na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu. 1

22Jua huchomoza, nao huondoka, 2 hurudi na kulala katika mapango yao. 1

23Kisha mwanadamu huenda kazini mwake, 2 katika kazi yake mpaka jioni. 1

24Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! 2 Kwa hekima ulizifanya zote, 2 dunia imejaa viumbe vyako. 1

25Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, 2 imejaa viumbe visivyo na idadi, 2 vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. 1

26Huko meli huenda na kurudi, 2 pia Lewiathani, + 104:26 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. uliyemuumba acheze ndani yake. 1

27Hawa wote wanakutazamia wewe, 2 uwape chakula chao kwa wakati wake. 1

28Wakati unapowapa, 2 wanakikusanya, 1 unapofumbua mkono wako, 2 wao wanashibishwa mema. 1

29Unapoficha uso wako, 2 wanapata hofu, 1 unapoondoa pumzi yao, 2 wanakufa na kurudi mavumbini. 1

30Unapopeleka Roho wako, 2 wanaumbwa, 2 nawe huufanya upya uso wa dunia. 1

31Utukufu wa Bwana na udumu milele, 2 Bwana na azifurahie kazi zake: 1

32yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka, 2 aigusaye milima, nayo ikatoa moshi. 1

33Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote; 2 nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi. 1

34Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, 2 ninapofurahi katika Bwana. 1

35Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia 2 na waovu wasiwepo tena. 1 Ee nafsi yangu, msifu Bwana. 1 Msifuni Bwana. + 104:35 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.

← Psalms 103Read In The App, Free →Psalms 105 →

Study Psalms 104

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150