Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 101

1Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako; 2 kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa. 1

2Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: 2 utakuja kwangu lini? 1 Nitatembea nyumbani mwangu 2 kwa moyo usio na lawama. 1

3Sitaweka mbele ya macho yangu 2 kitu kiovu. 1 Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; 2 hawatashikamana nami. 1

4Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; 2 nitajitenga na kila ubaya. 1

5Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri, 2 huyo nitamnyamazisha; 1 mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi 2 huyo sitamvumilia. 1

6Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, 2 ili waweze kuishi pamoja nami; 1 yeye ambaye moyo wake hauna lawama 2 atanitumikia. 1

7Mdanganyifu hatakaa 2 nyumbani mwangu, 1 yeye asemaye kwa uongo 2 hatasimama mbele yangu. 1

8Kila asubuhi nitawanyamazisha 2 waovu wote katika nchi; 1 nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya 2 kutoka mji wa Bwana.

← Psalms 100Read In The App, Free →Psalms 102 →

Study Psalms 101

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150