Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 57

1Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, 2 kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. 1 Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia 2 mpaka maafa yapite. 1

2Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, 2 Mungu atimizaye makusudi yake kwangu. 1

3Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, 2 akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; 2 Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. 1

4Niko katikati ya simba, 2 nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: 2 watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, 2 ambao ndimi zao ni panga kali. 1

5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, 2 utukufu wako na uenee duniani kote. 1

6Waliitegea miguu yangu nyavu, 2 nikainamishwa chini na dhiki. 1 Wamechimba shimo katika njia yangu, 2 lakini wametumbukia humo wao wenyewe. 1

7Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; 2 nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. 1

8Amka, nafsi yangu! 2 Amka, kinubi na zeze! 2 Nitayaamsha mapambazuko. 1

9Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; 2 nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. 1

10Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni, 2 uaminifu wako unazifikia anga. 1

11Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni, 2 utukufu wako na uwe duniani pote.

← Psalms 56Read In The App, Free →Psalms 58 →

Study Psalms 57

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150