Psalms 140
1Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu; 2 nilinde na watu wenye jeuri, 1
2ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao, 2 na kuchochea vita siku zote. 1
3Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, 2 sumu ya nyoka iko midomoni mwao. 1
4Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu; 2 nilinde na watu wenye jeuri 2 wanaopanga kunikwaza miguu yangu. 1
5Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa, 2 wametandaza kamba za wavu wao, 2 wametega mitego kwenye njia yangu. 1
6Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” 2 Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia. 1
7Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, 2 unikingaye kichwa changu siku ya vita: 1
8Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao, 2 usiache mipango yao ikafanikiwa, 2 wasije wakajisifu. 1
9Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe 2 na shida zinazosababishwa na midomo yao. 1
10Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! 2 Na watupwe motoni, 1 katika mashimo ya matope, 2 wasiinuke tena kamwe. 1
11Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; 2 maafa na yawawinde watu wenye jeuri. 1
12Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, 2 na kuitegemeza njia ya mhitaji. 1
13Hakika wenye haki watalisifu jina lako, 2 na waadilifu wataishi mbele zako.