Psalms 62
1Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; 2 wokovu wangu watoka kwake. 1
2Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; 1 yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe. 1
3Mtamshambulia mtu hata lini? 2 Je, ninyi nyote mtamtupa chini, 2 ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika? 1
4Walikusudia kikamilifu kumwangusha 2 toka mahali pake pa fahari; 2 wanafurahia uongo. 1 Kwa vinywa vyao hubariki, 2 lakini ndani ya mioyo yao hulaani. 1
5Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, 2 tumaini langu latoka kwake. 1
6Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; 2 ndiye ngome yangu, sitatikisika. 1
7Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, 2 ndiye mwamba wangu wenye nguvu 2 na kimbilio langu. 1
8Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote, 2 miminieni mioyo yenu kwake, 2 kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu. 1
9Binadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu, 2 nao wa ngazi ya juu ni uongo tu; 1 wakipimwa kwenye mizani, si chochote; 2 wote kwa pamoja ni pumzi tu. 1
10Usitumainie vya udhalimu 2 wala usijivune kwa vitu vya wizi; 1 ingawa utajiri wako utaongezeka, 2 usiviwekee moyo wako. 1
11Jambo moja Mungu amelisema, 2 mambo mawili nimeyasikia: 1 kwamba, Ee Mungu, 2 wewe una nguvu, 1
12na kwamba, Ee Bwana, 2 wewe ni mwenye upendo. 1 Hakika utampa kila mtu thawabu 2 kwa kadiri ya alivyotenda.