Psalms 60
1Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, 2 umekasirika: sasa turejeshe upya! 1
2Umetetemesha nchi na kuipasua; 2 uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka. 1
3Umewaonyesha watu wako nyakati za kukata tamaa; 2 umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha. 1
4Kwa wale wanaokucha wewe, 2 umewainulia bendera, 2 ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde. 1
5Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, 2 ili wale uwapendao wapate kuokolewa. 1
6Mungu amenena kutoka patakatifu pake: 2 “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi 2 na kulipima Bonde la Sukothi. 1
7Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; 2 Efraimu ni kofia yangu ya chuma, 2 nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. 1
8Moabu ni sinia langu la kunawia, 2 juu ya Edomu natupa kiatu changu; 2 nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” 1
9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? 2 Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? 1
10Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, 2 na hutoki tena na majeshi yetu? 1
11Tuletee msaada dhidi ya adui, 2 kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. 1
12Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, 2 naye atawaponda adui zetu.