Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 143

1Ee Bwana, sikia sala yangu, 2 sikiliza kilio changu unihurumie; 1 katika uaminifu na haki yako 2 njoo unisaidie. 1

2Usimhukumu mtumishi wako, 2 kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako. 1

3Adui hunifuatilia, 2 hunipondaponda chini; 1 hunifanya niishi gizani 2 kama wale waliokufa zamani. 1

4Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu, 2 moyo wangu ndani yangu unakata tamaa. 1

5Nakumbuka siku za zamani; 2 natafakari juu ya kazi zako zote, 1 naangalia juu ya kazi 2 ambazo mikono yako imezifanya. 1

6Nanyoosha mikono yangu kwako, 2 nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame. 1

7Ee Bwana, unijibu haraka, 2 roho yangu inazimia. 1 Usinifiche uso wako, 2 ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni. 1

8Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma, 2 kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako. 1 Nionyeshe njia nitakayoiendea, 2 kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. 1

9Ee Bwana, uniokoe na adui zangu, 2 kwa kuwa nimejificha kwako. 1

10Nifundishe kufanya mapenzi yako, 2 kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, 1 Roho wako mwema na aniongoze 2 katika nchi tambarare. 1

11Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu, 2 kwa haki yako nitoe katika taabu. 1

12Kwa upendo wako usiokoma, 2 nyamazisha adui zangu; 1 waangamize watesi wangu wote, 2 kwa kuwa mimi ni mtumishi wako.

← Psalms 142Read In The App, Free →Psalms 144 →

Study Psalms 143

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150