Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 89

1Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; 2 kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako 2 ujulikane kwa vizazi vyote. 1

2Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele 2 na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni. 1

3Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, 2 nimemwapia mtumishi wangu Daudi, 1

4‘Nitaimarisha uzao wako milele 2 na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ” 1

5Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, 2 uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu. 1

6Kwa kuwa ni nani katika mbingu 2 anayeweza kulinganishwa na Bwana? 1 Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni 2 aliye kama Bwana? 1

7Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, 2 anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka. 1

8Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 ni nani aliye kama wewe? 1 Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu, 2 na uaminifu wako unakuzunguka. 1

9Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; 2 wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza. 1

10Wewe ulimponda Rahabu + 89:10 Rahabu hapa ina maana jina la Misri kwa fumbo, yaani mwenye majivuno (lakini sio Rahabu wa Yos 2). 2 kama mmojawapo wa waliochinjwa; 1 kwa mkono wako wenye nguvu, 2 uliwatawanya adui zako. 1

11Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, 2 uliuwekea ulimwengu msingi 2 pamoja na vyote vilivyomo. 1

12Uliumba kaskazini na kusini; 2 Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha. 1

13Mkono wako umejaa uwezo; 2 mkono wako una nguvu, 2 mkono wako wa kuume umetukuzwa. 1

14Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; 2 upendo na uaminifu vinakutangulia. 1

15Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, 2 wanaotembea katika mwanga 2 wa uwepo wako, Ee Bwana. 1

16Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, 2 wanafurahi katika haki yako. 1

17Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, 2 kwa wema wako unatukuza pembe + 89:17 Pembe inawakilisha nguvu. yetu. 1

18Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, 2 na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1

19Ulizungumza wakati fulani katika maono, 2 kwa watu wako waaminifu, ukasema: 1 “Nimeweka nguvu kwa shujaa, 2 nimemwinua kijana miongoni mwa watu. 1

20Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, 2 na nimemtia mafuta yangu matakatifu. 1

21Kitanga changu kitamtegemeza, 2 hakika mkono wangu utamtia nguvu. 1

22Hakuna adui atakayemtoza ushuru, 2 hakuna mtu mwovu atakayemwonea. 1

23Nitawaponda adui zake mbele zake 2 na kuwaangamiza watesi wake. 1

24Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, 2 kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa. 1

25Nitauweka mkono wake juu ya bahari, 2 mkono wake wa kuume juu ya mito. 1

26Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, 2 Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’ 1

27Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, 2 aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia. 1

28Nitadumisha upendo wangu kwake milele, 2 na agano langu naye litakuwa imara. 1

29Nitaudumisha uzao wake milele, 2 kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu. 1

30“Kama wanae wataacha amri yangu 2 na wasifuate sheria zangu, 1

31kama wakihalifu maagizo yangu 2 na kutoshika amri zangu, 1

32nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, 2 uovu wao kwa kuwapiga, 1

33lakini sitauondoa upendo wangu kwake, 2 wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe. 1

34Mimi sitavunja agano langu 2 wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka. 1

35Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, 2 nami sitamdanganya Daudi: 1

36kwamba uzao wake utaendelea milele, 2 na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua; 1

37kitaimarishwa milele kama mwezi, 2 shahidi mwaminifu angani.” 1

38Lakini wewe umemkataa, umemdharau, 2 umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako. 1

39Umelikana agano lako na mtumishi wako, 2 na umeinajisi taji yake mavumbini. 1

40Umebomoa kuta zake zote, 2 na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu. 1

41Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake; 2 amekuwa dharau kwa jirani zake. 1

42Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, 2 umewafanya watesi wake wote washangilie. 1

43Umegeuza makali ya upanga wake, 2 na hukumpa msaada katika vita. 1

44Umeikomesha fahari yake, 2 na kukiangusha kiti chake cha enzi. 1

45Umezifupisha siku za ujana wake, 2 umemfunika kwa vazi la aibu. 1

46Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele? 2 Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini? 1

47Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka. 2 Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu! 1

48Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, 2 au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi? + 89:48 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 1

49Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni, 2 ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi? 1

50Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa, 2 jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote, 1

51dhihaka ambazo kwazo adui zako 2 wamenisimanga, Ee Bwana, 1 ambazo kwazo wamesimanga 2 kila hatua ya mpakwa mafuta wako. 1

52Msifuni Bwana milele! Amen na Amen.

← Psalms 88Read In The App, Free →Psalms 90 →

Study Psalms 89

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150