Psalms 5
1Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu, 2 uangalie kupiga kite kwangu. 1
2Sikiliza kilio changu ili unisaidie, 2 Mfalme wangu na Mungu wangu, 2 kwa maana kwako ninaomba. 1
3Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana; 2 asubuhi naleta haja zangu mbele zako, 2 na kusubiri kwa matumaini. 1
4Wewe si Mungu unayefurahia uovu, 2 kwako mtu mwovu hataishi. 1
5Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, 2 unawachukia wote watendao mabaya. 1
6Unawaangamiza wasemao uongo. 2 Bwana huwachukia 2 wamwagao damu na wadanganyifu. 1
7Lakini mimi, kwa rehema zako kuu, 2 nitakuja katika nyumba yako, 1 kwa unyenyekevu, nitasujudu 2 kuelekea Hekalu lako takatifu. 1
8Niongoze katika haki yako, Ee Bwana, 2 kwa sababu ya adui zangu, 2 nyoosha njia yako mbele yangu. 1
9Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, 2 mioyo yao imejaa maangamizi. 1 Koo lao ni kaburi lililo wazi, 2 kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu. 1
10Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu! 2 Hila zao ziwe anguko lao wenyewe. 1 Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi, 2 kwa kuwa wamekuasi wewe. 1
11Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi, 2 waimbe kwa shangwe daima. 1 Ueneze ulinzi wako juu yao, 2 ili wale wapendao jina lako 2 wapate kukushangilia. 1
12Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki, 2 unawazunguka kwa wema wako kama ngao.